Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Wakuu
Nimepitilia lineup za hivi vilabu vikubwa vya Simba na Yanga na kujiongea Utawala wa wachezaji wa kigeni katika vikosi vya kwanza vya Simba na Yanga, wakati Tanzania ikijiandaa kwa AFCON 2027, ni kisu chenye makali miwili. Kwa upande mmoja, nyota hawa wameiongezea Ligi Kuu ya NBC ushindani na thamani kubwa barani Afrika, huku wakiviwezesha vilabu kufanya vizuri kimataifa. Hata hivyo, ukweli mchungu ni kwamba wazalendo wengi wanaendelea kusukumwa benchi.
Hali hii ni tishio la moja kwa moja kwa Timu ya Taifa, Taifa Stars. Wachezaji wazawa wanakosa muda wa kucheza na uzoefu wa presha ya mechi kubwa. Vikosi vingi vinapoingia uwanjani, vimetawaliwa na wageni, jambo linaloweza mnyima kocha wa timu ya taifa chaguzi pana za wachezaji walio katika viwango vya ushindani.

Ili kunusuru jahazi, TFF na vilabu unadhani vifanye nini? Maana AFCON iko karibu na Wachezaji wa Taifa Stars ndio wapo kwenye vilabu hivi.
Pia soma ~ Miguel Gamondi: Uwepo wa wachezaji 12 wakigeni kwenye Ligi Kuu unapunguza nafasi ya kutosha kwa wachezaji wazawa