Wazazi acheni kulazimisha vijana wawatatulie changamoto zenu ambazo nyie mlishindwa kuzitatua kwa uzembe wenu

Kipondo Cha ugoko

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2023
Posts
878
Reaction score
1,511
Toka ujana wako wote mpaka unafikia umri huo hukujenga hata kichumba na kisebule eti unasubilia kijana wako uliemzaa asome kuanzia kindigate mpaka chuo, atafute ajira, ahangaike weee!! Ndo aje akujengee??? Aaahhh! Uzembe ulioje huo?

Yaani wewe miaka yote ya ujana wako mpaka unazeeka ulishindwa kujenga, Leo kijana kajitafuta weeee kapata visenti kidogo badala nae anze kupanga plan za maisha yake na familia yake eti unataka uanze kujengewa kwanza wewe(na pengine hata shule ulishindwa kumlipia Ada). Kasoma kwa kuunga unga mpaka kafika alipofika, wewe mzazi kusikia kijana kapata kijikazi tayari ushaanza kutaka utatuliwe shida zako zote ambazo wewe mwenyewe kwa uzembe wako ulishindwa kuzitatua kwa ujana wako wote.

Mzee unafikisha miaka50 huna hata kiwanja, huna hata shamba, ujana wako wote uliutumia vibaya kudhulura Kila mkoa bila tija yoyote, kula Bata, pombe na kubadiliaha wanawake ukasahau kwamba ujana ni mfupi kuliko uzee.

Sasa umri umeenda huna asset yoyote,huna kibiashara chochote unategemea vijana ambao ulisahau kuwajengea hata msingi kwa Kila hitaji lako. Aisee hii sio sawa

Kwa kuhitimisha niwashauri vijana wote ambao ndio wazee watarajiwa kwamba muda wa kuhakikisha Kila kitu kinakuwa sawa ni sasa, acha kuchezea pesa, hizo pesa unazochezea sasa Zina muda wake.

Now day tunakushauri kuhusu kutumia pesa vizuri unatujibu kwamba tuachane na maisha Yako! Mala "maisha ni Yako tushughulike na yetu" sawa tunakuacha lkn uzeeni hatutaki kutiliwa huruma na vijilawama uchwara. Ooohh! "Flani ana roho mbaya hataki kunisaidia" oooohh "jamaa anaringa kisa anavipesa n.k....
 
Kuna ukweli fulani yaani mzazi anaona kama ni lazima wewe kumtunza na kumfanyia mambo mengine ikiwa yeye yalimshinda,hicho kitu nimekiona pia.
Ila wengine walipambana yakagoma

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Watakuja hapa kusema "mzazi Ni mzazi yeye ndio kakuleta Duniani bila yeye wewe usingepata hata muda wa kununua simu kuja jf utasikia laana itakutafuna kama usipowasaidia wazazi " ....

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Toka ujana wako wote mpaka unafikia umri huo hukujenga hata kichumba na kisebule eti unasubilia kijana wako uliemzaa asome kuanzia kindigate mpaka chuo, atafute ajira, ahangaike weee!! Ndo aje akujengee??? Aaahhh! Uzembe ulioje huo?

Yaani wewe miaka yote ya ujana wako mpaka unazeeka ulishindwa kujenga, Leo kijana kajitafuta weeee kapata visenti kidogo badala nae anze kupanga plan za maisha yake na familia yake eti unataka uanze kujengewa kwanza wewe(na pengine hata shule ulishindwa kumlipia Ada). Kasoma kwa kuunga unga mpaka kafika alipofika, wewe mzazi kusikia kijana kapata kijikazi tayari ushaanza kutaka utatuliwe shida zako zote ambazo wewe mwenyewe kwa uzembe wako ulishindwa kuzitatua kwa ujana wako wote.

Mzee unafikisha miaka50 huna hata kiwanja, huna hata shamba, ujana wako wote uliutumia vibaya kudhulura Kila mkoa bila tija yoyote, kula Bata, pombe na kubadiliaha wanawake ukasahau kwamba ujana ni mfupi kuliko uzee.

Sasa umri umeenda huna asset yoyote,huna kibiashara chochote unategemea vijana ambao ulisahau kuwajengea hata msingi kwa Kila hitaji lako. Aisee hii sio sawa

Kwa kuhitimisha niwashauri vijana wote ambao ndio wazee watarajiwa kwamba muda wa kuhakikisha Kila kitu kinakuwa sawa ni sasa, acha kuchezea pesa, hizo pesa unazochezea sasa Zina muda wake.

Now day tunakushauri kuhusu kutumia pesa vizuri unatujibu kwamba tuachane na maisha Yako! Mala "maisha ni Yako tushughulike na yetu" sawa tunakuacha lkn uzeeni hatutaki kutiliwa huruma na vijilawama uchwara. Ooohh! "Flani ana roho mbaya hataki kunisaidia" oooohh "jamaa anaringa kisa anavipesa n.k....
Kwenye dini ya kiislamu tunafundishwa kua unavyomiliki wewe mtoto vyote ni vya baba ako na huna pingamizi lolote juu ya hilo

Subiri uanze kulea japo katoto kamoja ndo utajua maana ya Mzazi
 
Huu ukweli watu wengi hawaupendi. Ila ukiwa na nafasi ya kusaidia wazazi wako wasaidie mimi nashukuru Mungu aliwachukua nikiwa mtoto maana wangepata tabu sana kama wangekuwa wananitegemea mm, ningekuwa nawasaidia kila mwaka ambao kombe la dunia linacheza. 🤣
 
Back
Top Bottom