Wazazi hebu leteni maoni yenu hapa

Wazazi hebu leteni maoni yenu hapa

Extrovert

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2016
Posts
70,785
Reaction score
186,690
Ikiwa mzazi ambaye anamuwazia mazuri mtoto akimaliza elimu yake ya juu kwa atatumia mahela kibao kugharamia elimu ya mtoto ila by the end!

1. Mtoto anatakiwa akanunuliwe mashine ya popcorn aiweke stand aanze kuuza bisi!

2. Anunue mashine ya kukamulia juisi ya miwa na glass!

3. Aanze kuuza uji kwa kutembeza machupa vijiweni huko.

4. Aanze kubeba zege na usaidia fundi.

5. Aanze kuuza pweza na uduvi maeneo ya stendi!

6. Anunuliwe jiko la mkaa la size ya kuchomea mahindi ya kuchoma aanze kuuza mahindi!

7. Awe mpiga debe stand za vidala dala aunge unge mia mia!

Hapa jukwaani kuna wazazi wengi bila shaka wenye watoto wadogo say 1-8 years! Mnalipa ada kubwa tu watoto wakiwa junior schools 2-3 million per annum! Je, hiki ndio hasa ambacho mtapenda watoto wenu wafanye wakimaliza elimu zao za juu!

Hebu lets be frank guys! Lawama zimekuwa nyingi mno kwa hawa graduates kana kwamba nyie hamna watoto wadogo humo majumbani ambao watakuta the situation is even worst. Hamna ambaye hataki mwanae ale pazuri!
 
Mkuu umeongea ukweli kabisa, mimi mwanangu wa kwanza ana miaka 6, ndiyo yuko la kwanza ila nikiwaza karo ninayomlipia shule ukweli ninalipa aje kuwa mtu flani siyo aje tena kutembeza mandazi.

Jambo ninalowaza Mungu anijalie nikuze kampuni wanangu waje kuwa waendesha kampuni kama wafanyavyo wahindi. Kwamba mtoto anasoma anarudi kuendeleza biasara ya familia.

Tofauti na hapo unaweza kuchoma pesa tu.
 
Una point but my concern ni moja wakati unaandaa hayo yote umeshawahi kupata wasaa wa kufatilia kwa ukaribu talents za mtoto wako?

What if ana ndoto za kuwa mwanamuziki au kucheza football au basketball?what if anataka awe the next hashim thabeet au diamond?au awe kama sama goal?unadhan kumfundisha kuuza maandazi nae hana hizo ndoto kutamfaa au kutaua talent yake?

Nadhan wazazi wanapaswa kujikita katika kufahamu talent za watoto na kuziendeleza,si watoto wote wanaweza kufanya biashara!we are born differently inside and out!

Haya ni mawazo yangu tu though
 
Kwani nini Maana ya elimu?

Mkuu kwani kuuza pweza sio biashara? Kuuza juice sio biashara? Kuuza popcorn sio biashara?

Kinacho takiwa ni malengo ya muhusika, je ana malengo yapi na biashara ya Juice? Anataka kufika wapi?

Vipi akiajiriwa na mkamua Juice ya miwa hapo ni powa?

Bado sana sisi
 
Mkuu umeongea ukweli kabisa, mimi mwanangu wa kwanza ana miaka 6, ndiyo yuko la kwanza ila nikiwaza karo ninayomlipia shule ukweli ninalipa aje kuwa mtu flani siyo aje tena kutembeza mandazi...
Mkuu Bagharesa si anazalisha Mandazi? Kule Arusha wakian Sankist wahindi wale wanazalisha mandazi na mikate na wameajiri wasomi.

Vipi akiajiriwa kwenye kiwanda cha kuzalisha mandazi na akawa sales man?
 
Ninachokifanya kama mzazi ni kutafuta watoto warithi utajiri.
elimu ibakie status ambayo itawasaidia katika kuwa na exposure na kupanua fikra zao,

ila kusema tu unalipa ada then the rest you leave to the kids and government ni kuchimba kaburi mapemaa
 
Hapa ndo Pale Wahindi hasaa wanapo tupigia fimbo, Kuna Muhindi Arusha Jamaa kasoma MBA India baadae karudi Arusha ni kwao sasa alianza na kijiwe cha kuuza juice mbali mbali mimi nilijuana naye kwa sababu nilikuwa na muuzia Strawberry nilikuwa nachukua Nairobi nampelekea, akawa rafiki sana, na kuna wakati alikuwa ananituma hadi Nairobi naenda kuchukua aina fulani za matunda ya juice.

Siku hakuna wateja tunapiga story ndo kujua kasoma India MBA, kwa sasa ana Min Super amarket na ifanya vizuri sana na still ana process na juice na Bite ana tengeneza, Ile Super Market yake huwa ana fight sana anapata tenda za kufunga bidhaa za Hoteli huko Polini,

Sasa sisi tuendelee kusema ni kazi za aibu.
 
Mkuu Bagharesa si anazalisha Mandazi? Kule Arusha wakian Sankist wahindi wale wanazalisha mandazi na mikate na wameajiri wasomi.

Vipi akiajiriwa kwenye kiwanda cha kuzalisha mandazi na akawa sales man?
Hayo mandaz hayazalishwi kwa style ya kumaliza chuo ukaanza na mtaji wa 50,000 mkuu. Hivyo vifaa vya kuzalishia maandazi hao wahindi na bakhresa ni mtaji tosha, hata kuyasambaza wanatumia magari.
Mimi nilimaanisha mandazi ya mtaji mdogo haya ya mtaani kwetu.
 
Nilienda nae kanisani siku moja ... Kuna vyombo vingi Sana vya music .. Kuanzia
Piano.
Guitars
Drums
Trumpets..
Mda wote wanakwaya walipokuwa wakiimba alikuwa akisema baba nataka niende pale .. nataka ... Nikamwambia subiri ibada iishe utaenda mwanangu .. tukikaa mpaka ilipoisha .. Wanakwaya walikuwa pale plus Wale wapiga Tarumbeta ngoma etc .. Straight alienda kwenye piano .. just playing ... Akaemda kwenye 🥁 Piga piga Sana pale.. lately Akaomba Tarumbeta akajitutumua akapuliza sauti ikatoka..
Nyumbani Ni music music na yeye..
Kudance na kuimitate upigaji wa ala za music..
Mama yake hataki afanye hivyo ati atakuwa muhuni..
Nilichoamua Sasa hivi Yuko huko day care anahangaika na hesabu na mwandiko.. next year ..nampeleka shule ya music Kama budget itakuwa vizuri .. au atakuwa anakwenda kanisani kujifunza..
Shule zetu nyingi haziendelezi vipaji vya watoto ,zinamkaririsha masomo tuu Basi ...
Talents zinakuwa nurtured kuanzia early stages ...
Mtoto anaanza kuonyesha talents since mdogo kabisa jee sisi wazazi tuna ujuzi wa kunurture hizo talents ziwe ji zenye manufaa Sasa na hapo baadae?
Shule zetu za watoto almaarufu Kama daycares Zina facilities za kunurture Vipaji vya wanetu?
Ama ndo numbers numbers mpaka kieleweke.
I stand to be corrected.
 
Ninachokifanya kama mzazi ni kutafuta watoto warithi utajiri.
elimu ibakie status ambayo itawasaidia katika kuwa na exposure na kupanua fikra zao,

ila kusema tu unalipa ada then the rest you leave to the kids and government ni kuchimba kaburi mapemaa
Mawazo ya ajabu sana, huo urithi kama hawana akili ya kufight utaisha tu, wangapi waliachiwa urith na kwa sasa ni zero?
 
Hayo mandaz hayazalishwi kwa style ya kumaliza chuo ukaanza na mtaji wa 50,000 mkuu. Hivyo vifaa vya kuzalishia maandazi hao wahindi na bakhresa ni mtaji tosha, hata kuyasambaza wanatumia magari.
Mimi nilimaanisha mandazi ya mtaji mdogo haya ya mtaani kwetu.
Hahaa kwa hio kinacho dhalilisha ni kwa sababu mtu kaanza na mtaji mdogo sio? Kumbe sio aina ya bidhaa? Hahaa kwamba kama ataanxs na mashine poa ila kama ataanza manualy hio sio poa

Aiseee Mungu atusaidie
 
Mkuu umeongea ukweli kabisa, mimi mwanangu wa kwanza ana miaka 6, ndiyo yuko la kwanza ila nikiwaza karo ninayomlipia shule ukweli ninalipa aje kuwa mtu flani siyo aje tena kutembeza mandazi.

Jambo ninalowaza Mungu anijalie nikuze kampuni wanangu waje kuwa waendesha kampuni kama wafanyavyo wahindi. Kwamba mtoto anasoma anarudi kuendeleza biasara ya familia.

Tofauti na hapo unaweza kuchoma pesa tu.
Wekexza kwenye biashara na watoto wasome kwa ajili ya business za familia
 
Hahaa kwa hio kinacho dhalilisha ni kwa sababu mtu kaanza na mtaji mdogo sio? Kumbe sio aina ya bidhaa? Hahaa kwamba kama ataanxs na mashine poa ila kama ataanza manualy hio sio poa

Aiseee Mungu atusaidie
Yani mkuu umsomeshe mtoto miaka zaidi ya 15 minimum ulipe milion 3 kwa mwaka halafu amalize aje aanze kuuza mandazi mtaji wa 50,000 kutoboa ni majaliwa.
Mkuu ikitokea imetokea kama hakuna option, ila kiuhalisia mimi kama mzazi ninayemsosha mtoto siyi target yangu.
Kama anataka uza mandazi walio nimpe mtaji wa kuwa na bakery ya kisasa aweze kufanya biashara kisasa.
 
Mawazo ya ajabu sana, huo urithi kama hawana akili ya kufight utaisha tu, wangapi waliachiwa urith na kwa sasa ni zero?
NEGATIVITY
umehesabu wenye mafanikio kutokana na urithi unaoanzia kwenye familia?
umekaa na wahindi japo kidogo ukaona how they run business as family?
 
Tustuke hizi shule za sst.zXimetufanyatuwe maskini tumewekeza sana ila outcome ni very marginal mm ninao wawili wanamaliza form form mwaka huu .... sijui kama wataenda mbele nafikiria wakasome ili wanasaidie kusimamia miradi yangu
 
Back
Top Bottom