Wazazi kamwe msiwaruhusu watoto wenu kuangalia filamu za kutisha (zombie & violent movies), kuna mkakati hatari wa shetani kwenye movie hizi!

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Same. Mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Majengo wilayani Same, mkoani Kilimanjaro Brian Elisha Godson (12) amejiua kwa kujinyonga akitaka kuigiza kama filamu ya kujinyonga aliyoipenda kuiangalia akiamini hatakufa.

Godson anadaiwa kufanya jaribio hilo kwa kujinyonga na shuka saa 12 asubuhi jana Jumamosi Septemba 30, mwaka huu, wakati bibi yake na ndugu zake wengine wakiwa wamelala.

Tukio hilo lilizua taharuki kubwa linatokea ikiwa zimepita siku 85 tangu rafiki yake na jirani yake Godson aitwaje Alex Mgonja mwanafunzi wa darasa la tano shule ya msingi ya Mtawa ya Mother Kelvin iliyopo Same kujinyonga kwa kutumia kitenge cha bibi yake aliyekuwa akiishi naye.

Bibi wa Godson, Endael Mhando, amesema mjukuuwake amekuwa akipenda kuangalia filamu za kutisha ‘Zombi’, akisema kuna siku moja alimweleza kuwa mtu anaweza kujinyonga na asife kutokana filamu hizo alizokuwa akiziangalia na wenzake.

“Alinambia kumbe unaweza kujaribu alafu ukatoka tuu vizuri, akanambia inawezakana yule mwenzetu aliyejinyonga ilikuwa ni bahati mbaya tuu maana kwenye filamu wanafanya hivyo lakini wanatoka na hawafi,”
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Yahaya Mdogo amesema uchunguzi unaendelea kuhusu tukio hilo.

Akizungumzia tukio hilo, mkuu wa wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amesema chanzo cha tukio hilo ni Godson amekuwa akipenda kuigiza filamu mbalimbali alizokuwa akipenda kuangalia kwenye runinga zinazohusu matukio ya kujinyonga.
Kasilda amesema matukio mengi yanayotokea wilayani humo kuhusu watoto imebainika kuwa wengi wao wanaishi na bibi zao, huku wazazi wengi hawako karibu na watoto wao, badala yake wapo mjini.

“Nitoe wito kwa wazazi kama ambavyo wamekuwa wakitafuta hawa watoto basi wajue wana haki ya kuwatunza na kuwalinda dhidi ya vitendo vinavowafanya watoe uhai wao.Hii imekuwa ni changamoto kubwa kwa watoto katika wilaya hii, wazazi wengi wameachia watoto bibi na babu zao

“Tutaandaa mpango wa kuangalia wa namna Serikali tunawasaka wazazi hawa ili kuwajibika kwa watoto wao, kwa sababu baadhi yao wanakaa bila wazazi wakati ni haki yao kulindwa,”amesema.

Mwananchi
 
Umauingizaje mkakati wa shetani hapo?

Kwa nini tusiseme tatizo ni wazazi kutolea watoto wao?

Kwa nini mkakati wa shetani usiwe kuzaa bila mpango wa kulea?
 
Shida ni kua jamii nzima ya kitanzania hatuna uelewa wa Parental Guidelines (PG)
Watengeneza muvi wala hawana shida maana muvi inakua ishawekewa Rankin zake kama iangaliwe watu miaka yote, 13PG au 16PG.

Sasa unaweza kuta mzazi anaangalia muvi yenye ranking ya TV-MA yupo pamoja na watoto. Au hajali watoto wanaangalia muvi yenye ranking gani. Hata Cartoon zina ranking yake sio kila katuni ni ya kuangalia mtoto. Kuna kama katuni za Adult Swim huko hakuna content za kitoto.
Nadhani elimu ndio inapaswa kutolewa kwa wazazi juu ya jambo hili. Mchawi wetu ni ujinga

Nishawahi ongea kuhusu hili..
 
Uko sahihi!..

Mfano dstv wakiweka movie wanaweka na angalizo la umri gani wa kuangalia hiyo movie.

Ila wabongo ndio hawajui
 
Same. Mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Majengo wilayani Same, mkoani Kilimanjaro Brian Elisha Godson (12) amejiua kwa kujinyonga akitaka kuigiza kama filamu ya kujinyonga aliyoipenda kuiangalia akiamini hatakufa.

Godson anadaiwa kufanya jaribio hilo kwa kujinyonga na shuka saa 12 asubuhi jana Jumamosi Septemba 30, mwaka huu, wakati bibi yake na ndugu zake wengine wakiwa wamelala.

Tukio hilo lilizua taharuki kubwa linatokea ikiwa zimepita siku 85 tangu rafiki yake na jirani yake Godson aitwaje Alex Mgonja mwanafunzi wa darasa la tano shule ya msingi ya Mtawa ya Mother Kelvin iliyopo Same kujinyonga kwa kutumia kitenge cha bibi yake aliyekuwa akiishi naye.

Bibi wa Godson, Endael Mhando, amesema mjukuuwake amekuwa akipenda kuangalia filamu za kutisha ‘Zombi’, akisema kuna siku moja alimweleza kuwa mtu anaweza kujinyonga na asife kutokana filamu hizo alizokuwa akiziangalia na wenzake.

“Alinambia kumbe unaweza kujaribu alafu ukatoka tuu vizuri, akanambia inawezakana yule mwenzetu aliyejinyonga ilikuwa ni bahati mbaya tuu maana kwenye filamu wanafanya hivyo lakini wanatoka na hawafi,”
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Yahaya Mdogo amesema uchunguzi unaendelea kuhusu tukio hilo.

Akizungumzia tukio hilo, mkuu wa wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amesema chanzo cha tukio hilo ni Godson amekuwa akipenda kuigiza filamu mbalimbali alizokuwa akipenda kuangalia kwenye runinga zinazohusu matukio ya kujinyonga.
Kasilda amesema matukio mengi yanayotokea wilayani humo kuhusu watoto imebainika kuwa wengi wao wanaishi na bibi zao, huku wazazi wengi hawako karibu na watoto wao, badala yake wapo mjini.

“Nitoe wito kwa wazazi kama ambavyo wamekuwa wakitafuta hawa watoto basi wajue wana haki ya kuwatunza na kuwalinda dhidi ya vitendo vinavowafanya watoe uhai wao.Hii imekuwa ni changamoto kubwa kwa watoto katika wilaya hii, wazazi wengi wameachia watoto bibi na babu zao

“Tutaandaa mpango wa kuangalia wa namna Serikali tunawasaka wazazi hawa ili kuwajibika kwa watoto wao, kwa sababu baadhi yao wanakaa bila wazazi wakati ni haki yao kulindwa,”amesema.

Mwananchi

Nafikiri mpango wa shetani
Kama huna ufahamu na mambo ya kiroho ni vigumu kuona hilo.

Naweza nikawa na uelewa wa kiroho kulilko mchungaji wako, Mkakati wa shetani upo katika kila tendo ovu duniani, the spirit behind ni ya shetani,:

  • Kwa nini mkakati wa shetani usiwe mzazi kupeleka mtoto kwa Bibi?
  • Kwa nini mkakati wa shetani usiwe labda kuna jirani mchawi kwa Bibi?
  • Kwa nini mkakati wa shetani usiwe kuzaa na kukwepa malezi?
  • Kwa nini mkakati wa Shetani usiwe kumtenga Mume na mke na wasimlee mtoto?

Wewe umekimbilia kwenye movie tu, kwa hiyo unatushauri tuzae, tupeleke watoto kwa Bibi zao halafu tutoe tv kwa sababu mkakati wa shetani upo kwenye films za kutisha?

Solution ya Mambo haya ni watu kumrudia Mungu, kwa ukamilifu, kumwomba na kukemea milango yote ya giza na mauti, huu ndo mwarobaini.

Unaweza kuta Bibi yake kamla kichawi, very possible, kabisa, kamemfaa, kakatoa Kafara, hata kama kusingekuwa na movie ya kutisha, kingetafutwa kingine.

Cha Muhimu, ni kumlingana Mungu na kuwa karibu na roho Mtakatifu ili uwe kujua hila za shetani na Mizizi ya matatizo.

Soma: 2 corithians 1.9 - 12
Romans: 1.14

Ongeza level yako ya uelewa hata kwa kusoma tu Biblia, itakusaidia.
 
Kama ni kuigiza wanayoyaona basi wangefanya mengi kupitia hii katuni

images - 2023-10-02T081635.294.jpeg
 
Mnapenda sana kumsingizia shetani ujinga wenu!kwanini usiwe mkakati wa Mungu?
 
Uko sahihi!..

Mfano dstv wakiweka movie wanaweka na angalizo la umri gani wa kuangalia hiyo movie.

Ila wabongo ndio hawajui
DSTV ya zaman 2010-2015 walikua wakiweka muvi wanasema kabisa kwa sauti "The following program is suitable for all age group" or "the following program is suitable for people with 16yrs" ila sasa hivi wanawake maneno tu. Na kingereza kwetu ni chenga.

Unakuta mzazi anaangalia Chanel ya wanyama simba anavyokula wanyama yupo na mtoto pembeni hawajui hata program za wanyama zina PG.
Wanachoelewa wazazi ni kua Maudhui ya ngono ndio hawatakiwi kutizama na mtoto, lakini kwenye muvi kuna mengi zaidi ya ngono ndio maana kuna kitu kinaitwa Restricted Rate (R-Rate). Mapigano,damu, dhamira ya muvi inaweza kua si nzuri kwa mtoto
 
Wabongo ni shida mkuu
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]dahh
 
Nafikiri mpango wa shetani

Naweza nikawa na uelewa wa kiroho kulilko mchungaji wako, Mkakati wa shetani upo katika kila tendo ovu duniani, the spirit behind ni ya shetani,:

  • Kwa nini mkakati wa shetani usiwe mzazi kupeleka mtoto kwa Bibi?
  • Kwa nini mkakati wa shetani usiwe labda kuna jirani mchawi kwa Bibi?
  • Kwa nini mkakati wa shetani usiwe kuzaa na kukwepa malezi?
  • Kwa nini mkakati wa Shetani usiwe kumtenga Mume na mke na wasimlee mtoto?

Wewe umekimbilia kwenye movie tu, kwa hiyo unatushauri tuzae, tupeleke watoto kwa Bibi zao halafu tutoe tv kwa sababu mkakati wa shetani upo kwenye films za kutisha?

Solution ya Mambo haya ni watu kumrudia Mungu, kwa ukamilifu, kumwomba na kukemea milango yote ya giza na mauti, huu ndo mwarobaini.

Unaweza kuta Bibi yake kamla kichawi, very possible, kabisa, kamemfaa, kakatoa Kafara, hata kama kusingekuwa na movie ya kutisha, kingetafutwa kingine.

Cha Muhimu, ni kumlingana Mungu na kuwa karibu na roho Mtakatifu ili uwe kujua hila za shetani na Mizizi ya matatizo.

Soma: 2 corithians 1.9 - 12
Romans: 1.14

Ongeza level yako ya uelewa hata kwa kusoma tu Biblia, itakusaidia.
Sijalimit kwamba upango wa shetani unaweza kuwa kwenye kila kitu ha jf yaweza pia kutumika ila nimekuwa specific kwenye movies kwa leo.
 
Halafu mtu anakuambia wazungu sio wachawi.
Hizo movies wangerekodi za Nini.
Wana hadi sikukuu kubwa ya wachawi inaitwa Halloween.
Huko CIA,KGB, Scotland Yard,kumejaa uchawi mtupu kwenye mission zao.
 
Kama huna ufahamu na mambo ya kiroho ni vigumu kuona hilo.
Achana na fikra za mambo ya kiroho.tatizo letu ni kukimbia malezi ya watoto wetu.tunataka wafundishwe na ulimwengu.Elimu ya kumfundisha mtoto ajitambue imekua haba ndo maana tunamsingizia shetani kwenye kila tatizo.
 
Batman, monster university, spider man, scoops doobu, cartoon za kwenye tv,kama umeamua kumuharibu mwanao mwache aziangalie,
Bora umdownloadie cartoon za kuchagua mwekee kwenye flash.
Spider man wanapromote ushoga cocomelon Wana katuni za mafundisho kwa watoto japo Kuna mwaka Kanisa Duniani liliwashutumu walitoa katuni ya kupromote ushoga.
 
Back
Top Bottom