Wazazi mmekuwaje?

Wazazi mmekuwaje?

ephen_

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2022
Posts
14,949
Reaction score
54,485
Habari!

Nilipomaliza chuo nilipatwa na mkasa. Ile nimemaliza tu mitihani nikamtaarifu mama, tukaongea tu vizuri kwa muda mfupi chumbani kwake, sasa wakati natoka nje akaniuliza swali 'kwahiyo ushapata mtu wa kukuoa?' moyo ulishtuka halafu chap nikaendelea na safari hapo nikajifanya sijamsikia.

Ikawa wimbo anaoupenda 'ushapata wa kukuoa? Nikawa namwambia sipo tayari kwa sasa nikimjibu hivyo anaanza kutoa risala 'unajua inabidi uolewe mimi najisikia vibaya kukuona tu hapa nyumbani'

Siku moja nikamwambia mimi sijapata hata wa kunioa, akasema 'uzuri wote huo hakuna aliyesema anataka kukuoa' ilibidi tu nicheke.

Ishapita miaka 3 tokea kisa hiki kitokea, juzi nikasema acha niwaulize wenzangu kama wanakutana na maswahibu kama yangu sababu huu wimbo mama yangu bado anauimba.

Rafiki yangu FLORA
Yeye aliniambia alivyomaliza Mitihani alichelewa kurudi nyumbani kwa miezi kadhaa, sasa kuna siku akaumwa akalazwa mama yake alivyoenda hospital akamkuta Flora yupo na boyfriend wake ila huyo bf akawapisha waongee.

Mama yake akamuuliza 'huyo kijana ni nani' Flora akamjibu ni rafiki yake.
Mama yake akamwambia bills ni kiasi gani ili alipie! Flora akamwambia 'rafiki yangu ameshalipia' mama yake akaguna.

Sasa Flora alivyorudi kwao, mama yake akaanza kuimba nyimbo kila mara 'Yule rafiki yako yuko wapi akuoe kuliko kushinda ndani kila siku' Flora akaishia tu kucheka.

Rafiki yangu REBECCA
Yeye alikuwa anabanwa sana, ni wale watoto geti kali. Alivyomaliza chuo kuna siku akamuomba mama yake ruhusa ya kwenda kumsalimia rafiki yake. Mama yake hakumuuliza maswali mengi kama alivyokua anafanya hapo awali.

Jioni mapema Rebecca aliporudi mama yake akamwambia 'Mbona umerudi mapema' akamjibu nilienda kumuona tu mara moja. Mama yake akamwambia 'Ebu tembeatembea wachumba wakuone sio kujifungia tu ndani'

Ila ameniambia huo wimbo mama yake aliuacha baada ya yeye kupata kazi.

Rafiki yangu ASHA
Huyu ndiye amenichekesha sana, anasema tulivyomaliza chuo baba yake akawa anamwambia 'fanya uolewe sitaki kukuona nyumbani kwangu'

Kuna siku akaenda kazini kwa baba yake akamkuta yupo na wanaume wengine akawasalimia.
Kijana mmoja akamwambia mzee wake kwamba hakujua kama ana binti mkubwa vile! Mzee wake akajibu 'Huyu ni binti yangu kamaliza chuo mwaka huu na bado hajaolewa' wote wakaishia kucheka.

Haikupita miezi mingi baba yake akamletea mchumba, ubani ukachomwa sasa hivi yupo kwenye ndoa.

Nilichokiona wazazi wengi ambao hawajajipata kazi wanayotupa watoto wa kike ni kuolewa tena kama mtoto hajapata kazi ya kufanya.

Ila ukiwa na kazi nzuri unapata pesa, hii risala ya kuolewa hawatoi hata ukifikisha miaka 40.

Sasa sijui wa kulaumiwa ni CCM, wazazi wetu au sisi watoto.
 
Sasa binti, we huoni tu dalili humu JF, binti akifika 30s wanavompopoa na wengi wanavokuja kutafuta waume humu?
Unaeza kulaumu au kuona wazazi wanaimba ngonjera lakini kaa ukijua kwa sisi wanaume, ni very rare kuoa mtu alie na umri mkubwa. Kwanza kuanzia 30s hata uzazi ni geriatrics.
Wasichana wana window flani between 24 and 28 years, hyo ndo window ambayo ni rahisi kuolewa lakn wengi hua hawaioni, ukishatoka hapo, utahaha kwa sababu ni rare kupata wa makamo yako.
Wengi watabisha, lakn ndo hali halisi.
Maybe kama uko huko mambele
 
Habari!
Nilipomaliza chuo nilipatwa na mkasa. Ile nimemaliza tu mitihani nikamtaarifu mama, tukaongea tu vizuri kwa muda mfupi chumbani kwake, sasa wakati natoka nje akaniuliza swali 'kwahiyo ushapata mtu wa kukuoa?' moyo ulishtuka halafu chap nikaendelea na safari hapo nikajifanya sijamsikia.

Ikawa wimbo anaoupenda 'ushapata wa kukuoa? Nikawa namwambia sipo tayari kwa sasa nikimjibu hivyo anaanza kutoa risala 'unajua inabidi uolewe mimi najisikia vibaya kukuona tu hapa nyumbani'
Siku moja nikamwambia mimi sijapata hata wa kunioa, akasema 'uzuri wote huo hakuna aliyesema anataka kukuoa' ilibidi tu nicheke mimi nilikua nishasoma akili yake kwamba uoga wa maisha unamsumbua

Ishapita miaka 3 tokea kisa hiki kitokea, juzi nikasema acha niwaulize wenzangu kama wanakutana na maswahibu kama yangu sababu huu wimbo mama angu bado anauimba

Rafiki yangu FLORA
Yeye aliniambia alivyomaliza Mitihani alichelewa kurudi nyumbani kwa miezi kadhaa, sasa kuna siku akaumwa akalazwa mama yake alivyoenda hospital akamkuta Flora yupo na boyfriend wake ila huyo bf akawapisha waongee
Mama ake akamuuliza 'huyo kijana ni nani' Flora akamjibu ni rafiki yake.
Mama ake akamwambia bills ni kiasi gani ili alipie! Flora akamwambia 'rafiki yangu ameshalipia' mama yake akaguna

Sasa Flora alivyorudi kwao, mama yake akaanza kuimba nyimbo kila mara 'Yule rafiki yako yuko wapi akuoe kuliko kushinda ndani kila siku' Flora akaishia tu kucheka.

Rafiki yangu REBECCA
Yeye alikua anabanwa sana, ni wale watoto geti kali. Alivyomaliza chuo kuna siku akamuomba mama yake ruhusa ya kwenda kumsalimia rafiki yake.
Mama yake hakumuuliza maswali mengi kama alivyokua anafanya hapo awali.

Jioni mapema Rebecca aliporudi mama yake akamwambia 'Mbona umerudi mapema' akamjibu nilienda kumuona tu mara moja
Mama yake akamwambia 'Ebu tembeatembea wachumba wakuone sio kujifungia tu ndani'

Ila ameniambia huo wimbo mama yake aliuacha baada ya yeye kupata kazi.

Rafiki yangu ASHA
Huyu ndiye amenichekesha sana, anasema tulivyomaliza chuo baba yake akawa anamwambia 'fanya uolewe sitaki kukuona nyumbani kwangu'
Kuna siku akaenda kazini kwa baba yake akamkuta yupo na wanaume wengine akawasalimia.
Kijana mmoja akamwambia mzee wake kwamba akujua kama ana binti mkubwa vile! Mzee wake akajibu 'Huyu ni binti yangu kamaliza chuo mwaka huu na bado hajaolewa' wote wakaishia kucheka.

Haikupita miezi mingi baba yake akamletea mchumba, ubani ukachomwa sasa hivi yupo kwenye ndoa.

Nilichokiona wazazi wengi ambao hawajajipata kazi wanayotupa watoto wa kike ni kuolewa tena kama mtoto hajapata kazi ya kufanya.
Ila ukiwa na kazi nzuri unapata pesa, hii risala ya kuolewa hawatoi hata ukifikisha miaka 40.

Sasa sijui wa kulaumiwa ni CCM, wazazi wetu au sisi watoto.
Hahahahaha, kuna wadada wanazekea nyumbani, wazazi hawataki hilo
 
Sasa muda wa mama yako kufaidi vitenge vya ccm umefika we si umekufa umeoza kwa Lucas Mwamshamba wewe
 
Back
Top Bottom