Wazazi mmekuwaje?

Wazazi mmekuwaje?

Umemaliza kila kitu. Hata mimi nina ushuhuda wa mabinti wengi wanaoishi kimaskini kwa kuharakia ndoa.
Hata sio mabinti peke yao. Vijana ambao tunatafuta bado nao waliokurupuka kuoa wanaonja joto la jiwe. Mtu kisa kamaliza chuo wazazi hao mbiombio wanataka aoe au kuolewa. Kuna washkaji zangu Waislamu wao wazazi wanaandaa mazingira kijana akimaliza ataoa na atamtunza mke kwa hiki kibiashara. Sunna haiji na maneno matupu.

Sasa wazazi wengine wanawaza kuchangiwa kurudishiwa michango yao ya harusi na kutuzwa, aftermath utajua wewe. Binti ni gratuate anaolewa na mume kaajiriwa Posta kwenye ofisi binafsi zile zinakaba unatumia muda mwingi kazini, take home 600,000 alafu wanaishi Mbezi ndanindani huko maana ndio nyumba nzuri zina gharama nafuu.

Ukitazama spending ya wote kwenye familia kwa mwezi ni 550,000 na hapo kuna miujiza mtoto haumwi. Akiumwa tu hizo nauli za Mbezi kwenda hospitali mke na mtoto hawapandi daladala ni bajaj. Hapo ukweni hawajafiwa na hawajapata harusi.

Vicious cycle of poverty.
 
Kuna binti nadhani mtakuwa mnalingana nae kamaliza degree miaka 4 iliyopita, alitaka sana kuolewa na milionea ili atukomeshe macuzooo ni wiki iliyopita tu kanipigia anatafuta mume walau mwenye elimu na kazi ya kuzugia,🤣🤣 anataka mbinu za kumnasa mwanaume wa kumpa heshima ya ndoa nyie dunia iko speed, yuko very desperate kwa sasa anahaha hadi huruma nyodo zote zimemuisha

Kama hauko tayari kuolewa baki hivyo hivyo ila huko mbeleni usije sumbua watu km huyo cuzo wangu
Kapeace naona unanichamba kiaina
Mimi nitaolewa ila sio sasa halafu hata sichagui sijui millionaire au kapuku muhimu nitimize ndoto zangu kwanza halafu ndo niungane na huyo Mr right
Umri wangu unaniruhusu cz hata baada ya miaka 5 mimi bado nitakua sijagusa 30😂
 
Kuna kijana hapo juu kasema Kila siku akija kwenu unamfungia vioo 😂😁😁😁
 
Habari!
Nilipomaliza chuo nilipatwa na mkasa. Ile nimemaliza tu mitihani nikamtaarifu mama, tukaongea tu vizuri kwa muda mfupi chumbani kwake, sasa wakati natoka nje akaniuliza swali 'kwahiyo ushapata mtu wa kukuoa?' moyo ulishtuka halafu chap nikaendelea na safari hapo nikajifanya sijamsikia.

Ikawa wimbo anaoupenda 'ushapata wa kukuoa? Nikawa namwambia sipo tayari kwa sasa nikimjibu hivyo anaanza kutoa risala 'unajua inabidi uolewe mimi najisikia vibaya kukuona tu hapa nyumbani'
Siku moja nikamwambia mimi sijapata hata wa kunioa, akasema 'uzuri wote huo hakuna aliyesema anataka kukuoa' ilibidi tu nicheke mimi nilikua nishasoma akili yake kwamba uoga wa maisha unamsumbua

Ishapita miaka 3 tokea kisa hiki kitokea, juzi nikasema acha niwaulize wenzangu kama wanakutana na maswahibu kama yangu sababu huu wimbo mama angu bado anauimba

Rafiki yangu FLORA
Yeye aliniambia alivyomaliza Mitihani alichelewa kurudi nyumbani kwa miezi kadhaa, sasa kuna siku akaumwa akalazwa mama yake alivyoenda hospital akamkuta Flora yupo na boyfriend wake ila huyo bf akawapisha waongee
Mama ake akamuuliza 'huyo kijana ni nani' Flora akamjibu ni rafiki yake.
Mama ake akamwambia bills ni kiasi gani ili alipie! Flora akamwambia 'rafiki yangu ameshalipia' mama yake akaguna

Sasa Flora alivyorudi kwao, mama yake akaanza kuimba nyimbo kila mara 'Yule rafiki yako yuko wapi akuoe kuliko kushinda ndani kila siku' Flora akaishia tu kucheka.

Rafiki yangu REBECCA
Yeye alikua anabanwa sana, ni wale watoto geti kali. Alivyomaliza chuo kuna siku akamuomba mama yake ruhusa ya kwenda kumsalimia rafiki yake.
Mama yake hakumuuliza maswali mengi kama alivyokua anafanya hapo awali.

Jioni mapema Rebecca aliporudi mama yake akamwambia 'Mbona umerudi mapema' akamjibu nilienda kumuona tu mara moja
Mama yake akamwambia 'Ebu tembeatembea wachumba wakuone sio kujifungia tu ndani'

Ila ameniambia huo wimbo mama yake aliuacha baada ya yeye kupata kazi.

Rafiki yangu ASHA
Huyu ndiye amenichekesha sana, anasema tulivyomaliza chuo baba yake akawa anamwambia 'fanya uolewe sitaki kukuona nyumbani kwangu'
Kuna siku akaenda kazini kwa baba yake akamkuta yupo na wanaume wengine akawasalimia.
Kijana mmoja akamwambia mzee wake kwamba akujua kama ana binti mkubwa vile! Mzee wake akajibu 'Huyu ni binti yangu kamaliza chuo mwaka huu na bado hajaolewa' wote wakaishia kucheka.

Haikupita miezi mingi baba yake akamletea mchumba, ubani ukachomwa sasa hivi yupo kwenye ndoa.

Nilichokiona wazazi wengi ambao hawajajipata kazi wanayotupa watoto wa kike ni kuolewa tena kama mtoto hajapata kazi ya kufanya.
Ila ukiwa na kazi nzuri unapata pesa, hii risala ya kuolewa hawatoi hata ukifikisha miaka 40.

Sasa sijui wa kulaumiwa ni CCM, wazazi wetu au sisi watoto.
Safari njema kwenye ndoa mkuu😁
 
Kuna binti nadhani mtakuwa mnalingana nae kamaliza degree miaka 4 iliyopita, alitaka sana kuolewa na milionea ili atukomeshe macuzooo ni wiki iliyopita tu kanipigia anatafuta mume walau mwenye elimu na kazi ya kuzugia,🤣🤣 anataka mbinu za kumnasa mwanaume wa kumpa heshima ya ndoa nyie dunia iko speed, yuko very desperate kwa sasa anahaha hadi huruma nyodo zote zimemuisha

Kama hauko tayari kuolewa baki hivyo hivyo ila huko mbeleni usije sumbua watu km huyo cuzo wangu
Hahahahaha, huyu alitakiwa ajazwe mimba kabisa
 
Kapeace naona unanichamba kiaina
Mimi nitaolewa ila sio sasa halafu hata sichagui sijui millionaire au kapuku muhimu nitimize ndoto zangu kwanza halafu ndo niungane na huyo Mr right
Umri wangu unaniruhusu cz hata baada ya miaka 5 mimi bado nitakua sijagusa 30😂
Samahani cuzo ni akina nani huko dasalamu?
 
Back
Top Bottom