Wazazi mmekuwaje?

Wazazi mmekuwaje?

Dada Kapeace heshima yako mkuu ,Mimi ni kijana mzee barobaro ,najipenda sana na naijua thamani ya mwanamke hasa tukija kwenye suala la kumpa zawadi na kumnunulia nguo hivyo najiona nafaa kuoa kabisa
Ni kijana mwenye kazi yake halali ya kiserikali huku kijijini ,naheshimika na diwani wa kata mpaka mtendaji wa kata ,kuhusu hela sio haba sikosi Mia tano tano za kunywa ulanzi popote niwapo .

Ila kikubwa Mimi ndiye mwenye gari aina ya Corolla hapa kijijini na ni hiyo itakodiwa kwaajili ya kampeni za uchaguzi hasa kwa diwani wetu maana ameanza kuniomba gari hili toka mwaka juzi ,
Natumai mpaka hapo Sina ugeni na wewe tena Ila nishajipambanua Kama mwanaume mwenye hadhi yake hapa kijijini Mpitulu tafadhali niunganishe na huyo cuzo wako nioe hata leo maana hela ya mandazi na kumuita shehe iko mfuko wa shati hapa si unajua nimepanda daraja ?

Nipichosahau ni kukuaambia kuwa Mimi ni mtoto wa mjini Dar es Salam tena mjini Kati nikikulia pale kwa miaka 35 nyuma hivyo inatoshaa kukuonesha kuwa nimesheheni sifa zote za mwanaume wa hadhi yake
Mama mkwe mlokole wale wa kufunga siku 7 za wiki hataki kuwasikia wavaa kanzu, binti akikosa mume miaka 2 hii naona anaenda kubaya sana
 
Mama mkwe mlokole wale wa kufunga siku 7 za wiki hataki kuwasikia wavaa kanzu, binti akikosa mume miaka 2 hii naona anaenda kubaya sana
Kwa nilipofikia hata kanisani nitaingia kusali ,kikubwa binti anipende na anijali tu ,umri unakimbia na wanakijiji niliwaahidi kuoa mwaka huu baada ya kikao Cha Kijiji kudai nawaharibia watoto wao
 
Habari!
Nilipomaliza chuo nilipatwa na mkasa. Ile nimemaliza tu mitihani nikamtaarifu mama, tukaongea tu vizuri kwa muda mfupi chumbani kwake, sasa wakati natoka nje akaniuliza swali 'kwahiyo ushapata mtu wa kukuoa?' moyo ulishtuka halafu chap nikaendelea na safari hapo nikajifanya sijamsikia.

Ikawa wimbo anaoupenda 'ushapata wa kukuoa? Nikawa namwambia sipo tayari kwa sasa nikimjibu hivyo anaanza kutoa risala 'unajua inabidi uolewe mimi najisikia vibaya kukuona tu hapa nyumbani'
Siku moja nikamwambia mimi sijapata hata wa kunioa, akasema 'uzuri wote huo hakuna aliyesema anataka kukuoa' ilibidi tu nicheke mimi nilikuwa nishasoma akili yake kwamba uoga wa maisha unamsumbua.

Ishapita miaka 3 tokea kisa hiki kitokea, juzi nikasema acha niwaulize wenzangu kama wanakutana na maswahibu kama yangu sababu huu wimbo mama yangu bado anauimba.

Rafiki yangu FLORA
Yeye aliniambia alivyomaliza Mitihani alichelewa kurudi nyumbani kwa miezi kadhaa, sasa kuna siku akaumwa akalazwa mama yake alivyoenda hospital akamkuta Flora yupo na boyfriend wake ila huyo bf akawapisha waongee.

Mama yake akamuuliza 'huyo kijana ni nani' Flora akamjibu ni rafiki yake.
Mama yake akamwambia bills ni kiasi gani ili alipie! Flora akamwambia 'rafiki yangu ameshalipia' mama yake akaguna.

Sasa Flora alivyorudi kwao, mama yake akaanza kuimba nyimbo kila mara 'Yule rafiki yako yuko wapi akuoe kuliko kushinda ndani kila siku' Flora akaishia tu kucheka.

Rafiki yangu REBECCA
Yeye alikuwa anabanwa sana, ni wale watoto geti kali. Alivyomaliza chuo kuna siku akamuomba mama yake ruhusa ya kwenda kumsalimia rafiki yake. Mama yake hakumuuliza maswali mengi kama alivyokua anafanya hapo awali.

Jioni mapema Rebecca aliporudi mama yake akamwambia 'Mbona umerudi mapema' akamjibu nilienda kumuona tu mara moja
Mama yake akamwambia 'Ebu tembeatembea wachumba wakuone sio kujifungia tu ndani'

Ila ameniambia huo wimbo mama yake aliuacha baada ya yeye kupata kazi.

Rafiki yangu ASHA
Huyu ndiye amenichekesha sana, anasema tulivyomaliza chuo baba yake akawa anamwambia 'fanya uolewe sitaki kukuona nyumbani kwangu'

Kuna siku akaenda kazini kwa baba yake akamkuta yupo na wanaume wengine akawasalimia.
Kijana mmoja akamwambia mzee wake kwamba hakujua kama ana binti mkubwa vile! Mzee wake akajibu 'Huyu ni binti yangu kamaliza chuo mwaka huu na bado hajaolewa' wote wakaishia kucheka.

Haikupita miezi mingi baba yake akamletea mchumba, ubani ukachomwa sasa hivi yupo kwenye ndoa.

Nilichokiona wazazi wengi ambao hawajajipata kazi wanayotupa watoto wa kike ni kuolewa tena kama mtoto hajapata kazi ya kufanya.

Ila ukiwa na kazi nzuri unapata pesa, hii risala ya kuolewa hawatoi hata ukifikisha miaka 40.

Sasa sijui wa kulaumiwa ni CCM, wazazi wetu au sisi watoto.
Sasa utaolewa vipi na PM umeifunga? Hebu fungua haraka wawekezaji wa ndani tuje kufanya uwekezaji haraka iwezekanavyo
 
Kwa nilipofikia hata kanisani nitaingia kusali ,kikubwa binti anipende na anijali tu ,umri unakimbia na wanakijiji niliwaahidi kuoa mwaka huu baada ya kikao Cha Kijiji kudai nawaharibia watoto wao
Tatizo nakusoma kiutani cuzo natamani asitirike kukwepa mabalaa, nilikuwa nasoma tu story za watu lakini nayashuhudia kwa macho yangu hali imebadilika sana,
 
Back
Top Bottom