Wazazi mmekuwaje?

Wazazi mmekuwaje?

Umedai sijasema uhalisia, nikakuuliza uhalisia ni upi. Ukaniuliza hoja yangu ni ipi.
Sasa ulijuaje sijasema uhalisia wakati hujajua hoja yangu ni ipi.

Unapinga jibu, unaulizwa kama hili sio jibu basi tupatie jawabu sahihi ili tujifunze. Unaanza kuuliza hivi swali lilikuwa ni nini.

Hoja kuu nimebainisha, unadai hujaiona ila hapa umeipinga⬇️⬇️

Hizo unazodai ni nadharia ndio uhalisia nilioona. Sasa nipe uhalisia wako mkuu, maana wangu umeita nadharia.
Suala la Ndoa na familia ni suala pana linalohitaji watu sahihi wa kuliendea. Hilo linafahamika.

Lakini Vijana Hawatakiwi Kukatishwa tamaa kuhusu kuwahi kuoa au kuolewa eti kwa sababu Familia ina Mambo mengi Na Gharama nyingi.

ETI wanatakiwa kuwa Stable kimaisha yaani awe na Nyumba Sijui Kiasi Furani as savings kwenye Accounts. Kiufupi mkiyasema hayo huwa Mnarejea maisha Ya Juu ambayo kiuhalisia Sio kila mtu anayaishi hayo katika jamii lakini maisha kwa watu wote yanaenda.

Sisemi kijana akurupuke aoe hata kama hana kitu chochote cha kumuingiza Kipato HAPANA. Lakini msi li over rate(Msilikuze mno) hilo jambo.

Unaweza ukasema Mtu aoe au aolewe akiwa Stable lakini maisha ni kushuka na kupanda bali kuna kuanguka kabisa jee ikitokea Mtu ameanguka katika maisha Amuache mkewe na watoto wake yaani aikimbie familia??

Hayo masuala ya Kuumwa watoto sijui mke sijui hili na lile ni mambo yapo katika jamii zetu tulizokulia (za kimasikini) Lakini sisi tumekuwa na Hadi leo tunadhubutu kuandika vitu kadhaa Kuhusu jamii lakini kama wazee wetu nao wangeamua kuwa na Maono kama yetu basi Jamii hii isingekuwa hivi ilivyo.

ndo maana nikakwambia Unachokizungumza ni nadharia lakini kiuharisia maisha hayaendi kwa mtazamo huo.


ZIPO FAIDA KADHAA ZA VIJANA WA KIKE NA WA KIUME(WALIOKIDHI VIGEZO) KUWAHI KUINGIA KATIKA NDOA (KUANZISHA FAMILIA).
 
Back
Top Bottom