Wazazi mmekuwaje?

Acha malalamiko binti, umefika muda, olewa au ondoka hapo nyumbani ukajitegemee. Wazazi wamechanga sana harusi na sendoff za watu. Ni muda wao nao kuitisha vikao, ebooo
 
Anaweza asiolewe ila washenzi wakamjaza mimba anatotoa watoto km kuku broiler hawana baba hapo hapo kwenu.
Miaka 25-30 fukuzilia mbali.
We unamjengea nyumba babaako na mama ila kuna litoto lipo linafukuliwa mitaro hapohapo nyumbani.
Hapo umekariri sio lazima kufanya hayo mapenzi , kujazwa mimba ni yeye ndio kataka
 
Sina mpango wa kuolewa, sifikirii hata kwa sasa
Yaani kuhusu ndoa mimi bado sana..!
Vp maswala yetu ya mengine... najua utando ulishatolewa pasina shaka.
 
Heshima ya Mwanamke yeyote hapa diniani ni KUOLEWA.

Kuna kitu labda wewe ephen_ na baadhi ya wanawake hamkijui vizuri, nitakufahamisha. Iko hivi;

MUNGU alimuumba Eva kwa lengo moja tu, la kuwa MKE wa Adamu. Hakukuwa na sababu nyingine zaidi ya hiyo.

Ukisoma Biblia utaona baada ya Eva kuumbwa BWANA MUNGU alimpeleka moja kwa moja kwa Adamu. Hakumpeleka sehemu nyingine youote ile ya Bustani bali alimpeleka pale alipo Adamu moja kwa moja.

Vivyo hivyo na ninyi Wanawake mmezaliwa ili muishi na Wanaume. Wewe ili ukamilike unapaswa kuwa na MUME.

Mama yako mzazi analitambua hilo na yuko SAHIHI kabisa kukukumbusha kuhusu kuolewa. Mwanamke hakuumbwa ili aishi peke yake hata kama ana pesa na mali zote za duniani bado ili akamilike kihisia na kimwili na kisaikolojia anahitaji MUME!

Tafiti mbalimbali zinaonesha Wanawake wanaoishi peke yao bila Mume wanapitia MSONGO MKUBWA wa mawazo maisha yao yote. Why? Because something is missing in their lives.

BWANA MUNGU alikutoa kwenye ubavu wa Mwanaume, hivyo ili ukamilike ni lazima uungane na MWANAUME. Kitendo cha kukutoa kwenye UBAVU wa Mwanaume kilikuwa na maana kubwa wala MUNGU hakufanya kwa kubahatisha.
 
Nimekuelewa vizuri sana!
Lakini tatizo lipo kwenye umri, wadau wanasema age ya 27+ ni ngumu kupata mtu wa kukuoa wakati mimi naona huo umri ndio sahihi mimi kuingia kwenye ndoa.
 
Nimekuelewa vizuri sana!
Lakini tatizo lipo kwenye umri, wadau wanasema age ya 27+ ni ngumu kupata mtu wa kukuoa wakati mimi naona huo umri ndio sahihi mimi kuingia kwenye ndoa.
27+ kwa Mwanamke ni umri mkubwa. Ukiolewa na 27+ unakuwa umebakiza 13 yrs kufika 40. Kipindi cha miaka 13 ni kifupi sana kwa Mumeo kukufurahia. Kipindi hicho utakuwa busy na masumbufu ya watoto, attention yako itakuwa kwa watoto na siku hazigandi ghafla miaka 40 hii hapa!
By the time unafika 40 unaanza kuzeeka automatically wakati huo Mumeo anawaona mabinti wadogo wenye 20yrs. Wewe tayari anakuona "Mzee" ndiyo hapo sasa unatafutiwa msaidizi kisirisiri.

Nikuambie kitu, mwanamke ili ufurahie maisha olewa ukiwa na 20 yrs to 23yrs.

Zaidi ya hapo ni stress tu.
 
Sasa nimegundua kua niolewe mapema ili nikazae mapema tupate muda mwingi wa kufurahi🙄
Maisha hayana formular atii! Sanasana kipindi hiki ambacho kila mtu anasumbuka na maisha.

Mimi nafata moyo wangu sababu kuna wengine wanaolewa na 20yrs ndoa inawashinda baada ya miaka 5 mwingine anaolewa na 30yrs na ndoa yake ina last.
 
Nimekuelewa vizuri sana!
Lakini tatizo lipo kwenye umri, wadau wanasema age ya 27+ ni ngumu kupata mtu wa kukuoa wakati mimi naona huo umri ndio sahihi mimi kuingia kwenye ndoa.
mwanamke hawezi kupanga ataolewa lini.

mimi nataka nikuoe mwaka huu alafu wew unasema hauko tayar hadi miaka 5 mbele nitakusubiria tuu kweli ?
Ni uongo...

labda mipango yako iendane na anaetaka kuoa kwa muda huo,
tofauti na hapo, muda wew upo tayari unakuta hamna wa kukuoa.
au unaolewa na mtu ilimradi tuu.

Kapeace amekupa mifano mizuri,

kaolewe mkuu mipango yako utatimiza tu hukohuko,

kwani usipoolewa ndo guarantee ya kutimiza malengo ?

feminists wanawaharibu
 
Ni kweli mkuu! Lakini kila mtu ana kitabu chake cha maisha na wala mimi sio feminist
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…