sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Sisemi kutoka kwenda mitaa ya mbali mbali kuzuruara mbali kama enzi zetu zamani, La hasha!! kwa sasa dunia imebadilika hivyo uhuru inabidi upungue lakini isiwe kuwanyima kabisa uhuru.
Ni vema uwe unamruhusu majirani marafiki zake wawe wanakuja kucheza nae kwako nae awe anaenda kwa marafiki zake wa jirani kucheza kwa sharti la kutoa taarifa mapema ili ujue sehemu alipo.
Hii mambo ya kufungia ndani watoto ni unyanyasaji, kumbuka huyo ni mtoto hivyo ni busara kumpa haki yake ya kuupitia utoto ila iwe chini ya uangalizi wako.
Unamzuia mtoto asitoke nje, huoni kwamba yupo hatarini kukosa uzoefu wa kujenga urafiki akaishia kuwa mtu anaependa kukaa pekeyake.
Unamfungia mtoto ndani awe anaangalia katuni ni nani kakwambia haya maisha yapo kikatuni katuni?
Unaogopa mtoto atapigwa na wenzie kwani sisi tulipokuwa watoto hatukupitia hivi vitu? Hata sisi tulipitia huko na tukajifunza mapema kujua kutatua hayo mambo aidha kwa kupambana nayo, kuyazuia, kujenga urafiki ili usaidiwe yakikukuta, n.k. Haya mambo hayakwepeki kwa kufungia ndani mtoto, yapo na atayakuta,
Maisha haya tumezungukwa na watu, huwezi fanya chochote bila watu, kuna watu wabaya na wazuri na kuwajua ni kwa kupata uzoefu wa kuishi nao na uzoefu huo kuupata ni lazima uishi nao, wazazi mnafungia watoto ndani waaicheze hata na wenzao majirani huu si uungwana.