Wazazi mnashirikiana na shule kuwatesa watoto

Wazazi mnashirikiana na shule kuwatesa watoto

City Owl

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
3,475
Reaction score
7,571
Wazazi, mnashirikiana na shule kuwatesa watoto.

Vitoto vyenyewe bado vidogo, miaka 11-13, vinaamshwa saa 10 au 11 alfajiri kuwahi shule. Wanawahi nini exactly?

Na bado watakaa shule mpaka saa 12 kisa remedials, kurudi nyumbani saa 1 jioni.. mtoto anafika hoi, hajiwezi, hajacheza, hajafanya hobby zake. Kateseka tu.

Yote kwa faida gani?

- Mitihani ya darasa la saba haina umuhimu tena kama ilivyokuwa.
Wenye shule wanawatumia watoto wetu ku-market shule zao ili waonekane wana average ya A, ilhali hata kwa C mtoto anaenda zake secondary school. Au mnataka wakasome St. Francis na Marian? Shule zipo tu. Waliosoma huko si tumewaona chuo na mitaani tunao.

- Masomo ya ziada si kwa kila mwanafunzi kama ambavyo hizi shule zimewaaminisha. Mwanao kipanga, remedials za nini?
Acha wanaostruggle ndo wapambane.
Obviously, wanaunda tu room ya kupiga hela ya michango ya hapa na pale.

Mwisho, tuache watoto wakue kwa amani. Hizo efforts tuzitie form 4 na kuendelea, watakuwa wamekuwa wakubwa na matokeo ya form 4 yana impact mpaka kwenye admission ya chuo, so ni muhimu. Siyo darasa la saba.
 
Hili limekua tatizo, mzazi anaishi Buhongwa mtoto anasoma Ilemela.
School bus linampitia sa kumi na moja na dk 07, sa sijui anaamka muda gani

Au unakuta katoto kako darasa la tatu kako boarding school.
Wazazi siku hizi wana roho mbaya
 
Umeandika point kubwa sana mkuu inafikia hatua mpaka jumapili watoto wanatakiwa waende shule nadhani hii ni kuwafaidisha walimu zaidi na pesa za mikakati na mitihani isiyo na faida .
Yaani weekend wanaenda shule, likizo wananyimwa..
Halafu mambo yenyewe wanayokaririshwa huko mashuleni ni 'What's the name of the Zaramo traditional dance ?' au ' When was IBEACO established?' watoto wa 2012/13 hawa wanakaririashwa kampuni za wakoloni zilianzishwa lini.. hata waingereza wenyewe hawasomi huo upuuzi tena.
 
Shule ya itumba sekondari iko wilaya ya Ileje,form two eti wanaenda asubuhi Hadi Saa mbili usiku. Hapo wazazi tutegemee mimba Kwa mabinti zetu. Binti anafika nyumban almost Saa tatu usiku. Nawaza San na huku kuna visa vingi Sana vya ubakaji.
 
Back
Top Bottom