Wazazi mnashirikiana na shule kuwatesa watoto

Wazazi mnashirikiana na shule kuwatesa watoto

Shule zinavunja sheria nyingi sana, zinawafanya watoto watumwa wa elimu na sisi wazazi tuna comply kila wanachosema.

Mtoto anaendaje shule saa 11 alfajiri, unamplelekaje mtoto wa la nne boarding school? Mimi sitakubali hata kidogo.
 
Yaani weekend wanaenda shule, likizo wananyimwa..
Halafu mambo yenyewe wanyokaririshwa huko mashuleni ni 'What's the name of the Zaramo traditional dance ?' au ' When was IBEACO established?' watoto wa 2012/13 hawa wanakaririashwa kampuni za wakoloni zilianzishwa lini.. hata waingereza wenyewe hawasomi huo upuuzi tena.
Hapa naona shida sio mtoto wala mzazi😂😂
 
Mtoto
Shule ya itumba sekondari iko wilaya ya Ileje,form two eti wanaenda asubuhi Hadi Sana mbili usiku. Hapo wazazi tutegemee mimba Kwa mabinti zetu. Binti anafika nyumban almost Saa tatu usiku. Nawaza San na huku kuna visa vingi Sana vya ubakaji.
Umefuatilia shule ukaambiwa kwamba wanatoka sana mbili au hiyo ratiba umepewa na mwanafunzi mwenyewe?kama ni mtoto kakupa ratiba jitahidi kufuatilia shule Ili upate ratiba kamili isijekuwa mtoto ndio tatizo.
 
Shule zinavunja sheria nyingi sana, zinawafanya watoto watumwa wa elimu na sisi wazazi tuna comply kila wanachosema.

Mtoto anaendaje shule saa 11 alfajiri, unamplelekaje mtoto wa la nne boarding school? Mimi sitakubali hata kidogo.
Mimi pia katoto kangu bado kana miaka 2, ila hakika sitakaa niruhusu huu upuuzi umkute.
 
Kabisa aisee.. Wazazi wengi wa Tanzania hawaelewi majukumu yao kwenye elimu ya mtoto past kulipa ada.
Yaani shule ikisema kitu, wazazi hawana la kubisha ilhali mzazi anawajibika kuamua welfare ya mtoto wake.
Kwahiyo wakiambiwa walete rambirambi ya mwenzao kafiwa mzazi akatae ama? Au kukiwa na birthday yake asiende na keki shule?
 
Mimi pia katoto kangu bado kana miaka 2, ila hakika sitakaa niruhusu huu upuuzi umkute.
Lazima wazazi tusimame kwenye nafasi yetu. Shule zenyewe gharama ni kubwa sana, lakini watafosi mambo mengi ili kuongeza gharama tu. J1 na J2 mtoto haendi shule, likizo mtoto apumzike ajifunze stadi zingine za maisha, hakuna kwenda boarding na hilo sitakubali.
 
Mtoto

Umefuatilia shule ukaambiwa kwamba wanatoka sana mbili au hiyo ratiba umepewa na mwanafunzi mwenyewe?kama ni mtoto kakupa ratiba jitahidi kufuatilia shule Ili upate ratiba kamili isijekuwa mtoto ndio tatizo.
Nimefuatilia mkuu eti madarasa ya mtihani yanabaki kujisomea....kuna wakati nawaza kumkataza nahisi nisije msababishia mwanangu unyanyapaa WA walimu. But sipendi huo utaratibu
 
Kwahiyo wakiambiwa walete rambirambi ya mwenzao kafiwa mzazi akatae ama? Au kukiwa na birthday yake asiende na keki shule?
Hapana. Hili si suala nalolisemea.
Hayo ni mambo ya kijamii yasiyo na shida.
Hoja ni watoto wamewekwa kwenye pressure kubwa kupindukia, wanatumikishwa kwenye mchakato wa kupata elimu. Yote, kwa faida ya shule.
 
Back
Top Bottom