Wazazi wanakimbizanq na shilingi..halafu imekuwa kama fasheni watoto kusoma English medium, imekuwa kama vile wazazi wanakwepa majukumu yao ya parenting..yani wanajitahidi wawe na mda mfupi na watoto wao..mda wote wawe shule, yani hata likizo hawataki wazazi wanawafukuzia watoto waende tuition, tena za kuchelewa kurudi, yani mzazi kamwachia mwalimu ajipigiage hela, na walimu wanafurahi maana wako busy na kutoa maswali na kusahihisha, wanashinda shuleni...elimu gani, ipi, inafaa nini? Tumesoma zamani no tuition no what ila hatukuwa worse!! Sikatai ulimwengu uko mbio sana ila malezi mhimu pia, tusiwaachie walimu pekee..kama ni likizo it's time for parents or guardians to have their time for their children, kuwapa yale ya nje ya mtaala wa shule,...mda wa kusoma shuleni uheshimiwe na watoto warudi nyumbani in good time, watoto wadogo chini ya miaka 10 parenting iwe closer na wazazi, wasome shule za karibu ili wasidamke sana japo ni kawaida kuanzia saa 12 lakini sio saa 10 alfajili, ni kuwatesa..pia watoto kuanza shule hata maneno hayajajiumba vema mdomoni, akili bado tunataka kuwahisha shule kwa visababu vingii eti awahi kumaliza masomo..unadhani waliosema aanze la kwanza miaka 6 au 7 walikuwa hawana akili, au kwakuwa tunasema watoto wasasa wanakua haraka? Hapana!!