Wazazi mnashirikiana na shule kuwatesa watoto

Wazazi mnashirikiana na shule kuwatesa watoto

Kuna kipindi nilikuwa namuamsha mwanangu saa kumi na moja, yaaani anaandaliwa sare anavalishwa anasinzia, chai anakunywa hawezi anasinzia kikombe mdomoni achilia mbl baridi kali ya umande iliyokuwepo!!!

Nikaona hii nikumtesa mtoto daah mpk roho ilikuwa inauma 😁😁😁
Nikaachana na huo ujinga
 
Kwanza mabegi ni makubwa...wanaweka nini?? Sisi tumesomea adidas daftar 4 tu zinatosha...kwa kifupi elimu imekuwa biashara sana...

NB : hongera mtoa mada umewaza mbali sana.
 
Kwanza mabegi ni makubwa...wanaweka nini?? Sisi tumesomea adidas daftar 4 tu zinatosha...kwa kifupi elimu imekuwa biashara sana...

NB : hongera mtoa mada umewaza mbali sana.
Ahsante mkuu.
Mabegi makubwa na mazito.. mtoto ana madaftari na vitabu vya masomo 6 ya wizara, na bado shule imeongeza French, ICT, dini au/na Entrepreneurship..
Mitaala inayotambulika duniani kama Cambridge International wanfocus na masomo 3 tu - English, Math and Science kwa level ya primary, na ndiyo wanafanyia mitihani ya kuhitimu primary school.
 
Wazazi, mnashirikiana na shule kuwatesa watoto.

Vitoto vyenyewe bado vidogo, miaka 11-13, vinaamshwa saa 10 au 11 alfajiri kuwahi shule. Wanawahi nini exactly?
Na bado watakaa shule mpaka saa 12 kisa remedials, kurudi nyumbani saa 1 jioni.. mtoto anafika hoi, hajiwezi, hajacheza, hajafanya hobby zake. Kateseka tu.

Yote kwa faida gani?

- Mitihani ya darasa la saba haina umuhimu tena kama ilivyokuwa.
Wenye shule wanawatumia watoto wetu ku-market shule zao ili waonekane wana average ya A, ilhali hata kwa C mtoto anaenda zake secondary school. Au mnataka wakasome St. Francis na Marian? Shule zipo tu. Waliosoma huko si tumewaona chuo na mitaani tunao.!

- Masomo ya ziada si kwa kila mwanafunzi kama ambavyo hizi shule zimewaaminisha. Mwanao kipanga, remedials za nini?
Acha wanaostruggle ndo wapambane.
Obviously, wanaunda tu room ya kupiga hela ya michango ya hapa na pale.

Mwisho, tuache watoto wakue kwa amani.
Hizo efforts tuzitie form 4 na kuendelea, watakuwa wamekuwa wakubwa na matokeo ya form 4 yana impact mpaka kwenye admission ya chuo, so ni muhimu. Siyo darasa la saba.
Ujinga mtupu, ukiwa na pesa Peleka watoto Internationa School, Hizi English Medium ni uhuni mkubwa na hakuna kitu pale, watu tunapigwa mchana kweupe
 
Umeandika point kubwa sana mkuu inafikia hatua mpaka jumapili watoto wanatakiwa waende shule nadhani hii ni kuwafaidisha walimu zaidi na pesa za mikakati na mitihani isiyo na faida .
Ni ujinga, ndio maana huwa nasema kila siku kama mtu unapesa peleka watoto Internation school basi, hizi Englisg Medium ni uhuni hakuna elimu pale. tutaelewa siku moja.
 
Shule zinavunja sheria nyingi sana, zinawafanya watoto watumwa wa elimu na sisi wazazi tuna comply kila wanachosema.

Mtoto anaendaje shule saa 11 alfajiri, unamplelekaje mtoto wa la nne boarding school? Mimi sitakubali hata kidogo.
Violation of human rights.

Unamnyima mtoto haki ya kulala na kupumzika ipasavyo
 
Inasikitisha sana na stil bado wanapewa na Homework maswali kama 50 na mzazi anatamba mtaa mzima mtoto wake anasoma shule nzuri. Mtoto yuko Baby class anapewa Homework maswali 50+ maswali yenyewe ya kijinga jinga tupu.
Baby class na home work ya maana 🤣🤣🤣
 
Mitaala inayotambulika duniani kama Cambridge International wanfocus na masomo 3 tu - English, Math and Science kwa level ya primary, na ndiyo wanafanyia mitihani ya kuhitimu primary school.
Huu mfumo ungekuwepo bongo tungefika mbali , Tatizo wazazi hawasupport Mabadiliko yoyote wenyewe wanajua kuepeleka 2 watoto wadogo bweni yaani katoto kanaanzia chekechea hadi la saba bweni so 😭😭😭😭 sad
 
Nilipoona ajira ni kikwazo nchi hii hata kama ufaulu ni mzuri niliamua kijana wangu atasoma kayumba.
Huku kayumba hakuna changamoto kama hizo, remedials ninamuandalia mimi mwenyewe
Kayumba kuna elimu nzuri kuliko Englush Medium kama mtoti akiwa serious sema hatuelewi kabisa, Hakuna kitu huko English Medium, kama pesa zipo peleka International
 
Yaani weekend wanaenda shule, likizo wananyimwa..
Halafu mambo yenyewe wanyokaririshwa huko mashuleni ni 'What's the name of the Zaramo traditional dance ?' au ' When was IBEACO established?' watoto wa 2012/13 hawa wanakaririashwa kampuni za wakoloni zilianzishwa lini.. hata waingereza wenyewe hawasomi huo upuuzi tena.
Hakika....NCU,NMC,RETICO nk.watoto hawajui....na ..ndiyo CCM eti wanataka warejeshe vyama vya ushirika?: Watarajiwa wa kuvisimamia hawafundishwi vya awali ilikuwaje vikafa wajue na waweze kusahihisha makosa..
 
Huu mfumo ungekuwepo bongo tungefika mbali , Tatizo wazazi hawasupport Mabadiliko yoyote wenyewe wanajua kuepeleka 2 watoto wadogo bweni yaani katoto kanaanzia chekechea hadi la saba bweni so 😭😭😭😭 sad
Niliwahi kuuliza swi mahali kwamba hatuwezi copy mtala wa Internationl school na kuutumia shule za kawaida?
 
Back
Top Bottom