Wazazi mnashirikiana na shule kuwatesa watoto

Wazazi mnashirikiana na shule kuwatesa watoto

Ujinga mtupu, ukiwa na pesa Peleka watoto Internationa School, Hizi English Medium ni uhuni mkubwa na hakuna kitu pale, watu tunapigwa mchana kweupe
Na ukikutana na hao watoto wa English medium na vingereza vyao kule mlimani city utachoka
Waafrika tuna ushamba mwingi wa lugha. Mtoto anaongea English za kubumba na wazazi wengine unaona kabisa wanahangaika kuongea nao.
Mimi nafanya kazi na wafini, hawa watu wanapenda lugha yao hatari. Wanaongez English tukiwa pamoja, otherwise ni kilugha tu.
 
Hii kitu imenitesa sana mpaka o level... Af ukute hauna usafiri wowote... Mwalimu anahesabisha namba saa 12½ asubuhi... Kuna watu hawana huruma kbsa, kugonga viboko tu kufundisha aaaah
Hahahah. Walimu wengi wana matatizo ya akili. Viboko bila sababu za msingi. Mtoto kakosa swali, atapigwa hatari.
Kama haelewi ina maana hata wewe mwalimu uwezo wako wa kufundisha ni mdogo.
 
Na ukikutana na hao watoto wa English medium na vingereza vyao kule mlimani city utachoka
Waafrika tuna ushamba mwingi wa lugha. Mtoto anaongea English za kubumba na wazazi wengine unaona kabisa wanahangaika kuongea nao.
Mimi nafanya kazi na wafini, hawa watu wanapenda lugha yao hatari. Wanaongez English tukiwa pamoja, otherwise ni kilugha tu.
Ushamba sana ,mfano Watalii wanao kuja Tanzania huwa some time si kwamba hawajui Kingereza ila hawataki kuongea makusudi kabisa, Unakuta lazima uwatafutia tour guide wa Lugha yao na si kwamba Kingereza hawakijuia wanakijua sana. Mind set zetu ni za kimasikini si mind set za kutufanya tuwe Taifa kubwa.
 
Siku hizi watoto wa miaka 4 wana stress, sijhi miaka 20 ijayo tatizo la afya ya akili litakuwaje.

Katoto kanawaza kuwahi school bus, huku kina bag kubwa lina daftari 8 - 12 ni mateso bila chuki.

Hivi mtoto wa miaka 3 - 5 anaenda shule kujifunza nini hasa?, kwanini asibaki nyumbani akafundishwa msingi wa maadili ya kwao, akacheza na kugundua talanta yake.

Watu wengi wanawasomesha watoto na kusahau kuwalea watoto wao
 
Hao watoto wana wazazi, wazazi wameamu kufanya hivyo kwa watoto wao, hakuna shule inaweza amua kama mzazi hajaridhia.

Niliamua kuwa nawapeleka watoto shule asubuhi na kuwarudisha nyumbani, na hakuna ratiba ya ziada kwao.
 
NILIKATAA HUO UPUUZI,
ETI MTOTO SAA KUMI NA MBILI ASB AWE AMEFIKA SHULE, KUTOKA SAA KUMI NA MBILI JIONI.
KISA NI DARASA LA MTIHANI WA DARASA LA SABA AU LA NNE!

KILA BAADA YA MIEZI MIWILI MITATU, WATOTONAPELEKA HOPISTAL, KWA SBB YA UCHOVU NA MATONSEZI.
 
Aisee saa 10 unaenda wapi?
Kwa mtu ambaye anaishi Dar sidhani kama saa 10 ni usiku kwake.

Kuna siku nimetoka mkoani nikafika Stand ya Magufuri kama saa 8 hivi nilikuwa natakiwa Zanzibar saa 3 asbhi nikasema hapa silali niangaze angaze macho mazingira ya stand mara ghafra saa 10 alfajiri hii hapa nikasogea kwenye vituo vya daladala nikakuta kumeshakucha nyomi la watu wakiwemo Wanafunzi wanasubiri mwendokasi kutoka Mbezi na Mimi nikaungana nao.
 
Back
Top Bottom