Wazazi mnashirikiana na shule kuwatesa watoto

Hili suala limekosa utatuzi. Elimu Biashara ndo shida ya yote Haya..
 
Ulichoandika kilipaswa kiwe SHERIA siyo maoni.

Tatizo ni kutojali AZIMIO LA ARUSHA.

kipengere :- viongozi wa umma wasiwe na hisa katika makampuni.
 
Shule zinavunja sheria nyingi sana, zinawafanya watoto watumwa wa elimu na sisi wazazi tuna comply kila wanachosema.

Mtoto anaendaje shule saa 11 alfajiri, unamplelekaje mtoto wa la nne boarding school? Mimi sitakubali hata kidogo.
Kama unaweza fanya hivi:

Mtoto mpeleke hizi shule za serikali za kawaida tu, ukiona ana kichwa kizito mtafutie mwalimu awe anampiga Pindi home sa hivi walimu wapo wengi sana

Kama utashindwa hivyo mlipie masomo ya ziada kwenye shule ya Private(awe anahudhuria Tuition tu)
 
Mkuu umetiririka points za msingi tupu.
 
Mkuu umetiririka points za msingi tupu.
Hata tukitamani watoto wamalize masomo wakiwa na umri mdogo wapate ajira mapema, tukumbuke huko kwenye ajira kunataka upevu wa akili ya nje ya shule..sio GPA kubwa tu..kuna kijana aliajiliwa sehem akiwa na umri mdogo..yes!! pia na ufaulu mkubwa ..Yes, ila kazini utoto mwingi, ujana mwingi..mpaka maboss wake wakaona hafai..there is a time maturity ni mhimu kazini.
 
jitahidi kumpeleka mwanao shule ya maana..... elewa point (shule ya maana) usije ukachanganya shule ya bei ghali na shule ya maana.....

wazazi wengi wanafuata mkumbo hawachunguzi hawafuatilii nn mtoto anapata shuleni au shule ina program gani za kuchangamsha ubongo wa mtoto hayo mambo ya kukaa shule mpka sa 12 au kwenda mpka j2 kwangu sijawahi sikia na shule inafanya poa kama waalimu wakisimamia misingi ya kazi yao na kuweka juhudi kwenye kumuelewesha mtoto
 
Tatizo mfumo wetu wa elimu ni mbovu sana.Tungekuwa na mfumo mzuri watu wangesoma hizi za serikali ambazo unaenda asubuhi saa Moja na siyo huu upuuzi wa kuamushana saa kumi.wtz wanajikongija angalau ampeleke mwanae kwenye hivi vishule vya medium ili angalau ajue kidogo kiingereza tu basi hakuna kingine.
 
Shule ya itumba sekondari iko wilaya ya Ileje,form two eti wanaenda asubuhi Hadi Saa mbili usiku. Hapo wazazi tutegemee mimba Kwa mabinti zetu. Binti anafika nyumban almost Saa tatu usiku. Nawaza San na huku kuna visa vingi Sana vya ubakaji.
Kaka nsaidia mawasaliano yako n pm nataka kuhamia uko nadhani ntajua meng kuptia mwenyej
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…