Wazazi na Serikali tuangalie maadili ya watoto wetu Vyuo vya Kati

Wazazi na Serikali tuangalie maadili ya watoto wetu Vyuo vya Kati

guojr

Member
Joined
Dec 4, 2015
Posts
62
Reaction score
95
Kama wazazi au walezi tunapenda watoto wetu wapate elimu ili iwasaidie maishani mwao. Ila kuna hili jambo la wazazi na walezi kupeleka watoto wao kusoma kwenye hivi vyuo vya kati hasa hivi vinavyotambulika kama vyuo vya mipango ambavyo vipo mikoa mbalimbali. Watoto hawa wengine wakiwa chini ya miaka 18 pengine wakiwa bado wanahitaji malezi au uangalizi wa wazazi wao lakini wameachiwa kuishi maisha huru bila uangalizi wowote ni hatari kwa maisha yao ya baadae.

Watoto hawa wakiwa katika mazingira haya mapya na huru wanaweza kujifunza tabia mbalimbali nzuri na mbaya. Wengi wao bado wakiwa bado ni wadogo ki umri na kiakili wanaweza kujifunza mambo yasiyofaa ambayo yanaweza kufuta ndoto zao. Mtoto labda alikua akisoma shule ya bweni maisha yake yote au wazazi walikua wakimuangalia kwa ukaribu ila kumuacha mtoto kwenye mazingira haya yenye uhuru wa kila kila kitu unaweza kuchangia kumuaribu mtoto kitabia. Wawapo vyuoni wanakuatana na watu wenye tabia mbalimbali ila kibinadamu huwa wanavutiwa zaidi na mambo yasiyofaa kama ulevi, uzinifu na hata utumiaji wa madawa ya kulevya.

Watoto hawa wamekua rahisi kudanganyika na vitu vidogo, kama pesa, simu janja, nguo na kadhalika ambavyo vinaweza kuwashawishi kujiingiza kwenye ngono katika umri mdogo. Pia wanaweza kuashawishiwa na vijana wenzao au jamii inayowazunguka na kuwangiza katika tabia zisizofaa. Inauma sana kuona mtoto mdogo kabisa ametoka nyumbani huku wazazi wakiwa na matarajio makubwa na mtoto wao lakini anaporudi nyumbani anakua ameharibikiwa kabisa.

Wazazi na Serikali chukueni hatua mara moja kudhiti janga hili ili kudhibiti mmomonyoko wa maadili kwenye jamii, lakini pia kuwasadia wasije haribikiwa wakiwa wangali wadogo, nao wanamatarajio yao ya baadae. Kwa Serikali ningeshauri wangevifanya vyuo hivi kama shule ya sekondari nikimaanisha kuwe na sheria kali kama vile wapangiwe muda wa kuamka na kulala, wavae sare maalum, kurekodi mahudhurio na kadhalika.

Lakini pia kwa wazazi tuangalie maisha ya baadae ya watoto wetu, hautajisikia vizuri mwanao anarudi nyumbani ni mjamzito au mtumiaji wa madwa ya kulevya, ameathirika na magonjwa ya zinaa au amebadilika kabisa kitabia. Ningeshauri tusiwapeleke watoto wetu mbali ambapo hatuna njia ya kuwaangalia kwa ukaribu.

Nawasilisha.
 
Nafikiri mmomonyoko wa maadili umeanzia toka kwenye ngazi ya Familia. Sio jukumu la Serikali kuchunga vijana wetu.

Ili kupata mahitaji ya kifedha kumepelekea mabinti kutumia miili yao kama mtaji. Ila wengine wanabahatika kupata waume wa ukweli. Maana sehemu sahihi kwa binti msomi kupata Mume wa kufanana nae ni hapo Chuo sio mtaani.

Kwa Chuo nilichosoma Mimi niliona wasichana wote wa Darasa langu, kila Binti alipata Mpenzi. Pia kuna vijana walikuwa wanamiliki Mabinti 2 - 5 kwa wakati mmoja, wengine walikuwa na mahusiano na watu wa nje ya Chuo.

Mbaya zaidi nakumbuka tulikuwa tunasoma na Sista anasomeshwa na Kanisa, pia na yeye tukiwa mwaka wa mwisho nae alipata Mume na akaacha kabisa usista.
 
Mmmmmmhmn ila nadhani vyuo kama hivi inabidi kuwe na special regulations ambazo zitasaidia vijana wanapokuwa hapo vyuoni kitokuwa katika mazingira hatarishi.
 
Nafikiri mmomonyoko wa maadili umeanzia toka kwenye ngazi ya Familia. Sio jukumu la Serikali kuchunga vijana wetu.

Kwa Chuo nilichosoma Mimi niliona wasichana wote wa Darasa langu, kila Binti alipata Mpenzi. Pia kuna vijana walikuwa wanamiliki Mabinti 2 - 5 kwa wakati mmoja.
Na ni kama fasheni. Chuo binti akisema asiwe na mpenzi au awe bikra huwa ni mtihani mgumu sana kwake kusurvive hadi amalize chuo sababu ya peer pressure.

Marafiki huwa wanamsukumo mkubwa sana kumuamulia mtoto wa kike maisha yake anapokuwa chuo.

Wazazi ni vema kujenga utamaduni wa kuwa karibu na mabinti wanapokuwa vyuoni na ikibidi kuwatembelea mara kwa mara kuwatafutia sehemu ya kuishi salama na ikibidi wazazi mnaweza kuungana kushare cost za kodi na matunzo ya watoto sababu ya ugumu wa hali ya uchumi wa sasa.
 
Mambo ya ajabu yapo katika vyuo vyote na sio vyuo vya kati,akili za wanavyuo hazipishani sana hata wawe wamepevuka kwa kiasi gani,akishakua mwanachuo anafanana na waliomzunguka
 
Kwa jinsi jamii tulivyoharibikiwa thread hii itakuwa unpopular humu.

Vv
 
Ni kweli kabisa hawa wanaokwenda vyuo vya kati wengi ni wale waliomaliza form 4 ambao ndiyo kwanza wana miaka 18 wanachangamana na watu wa kila rika vyuoni
 
Inashangaza sana binti mdogo hana ajira mwanafunzi anamiliki simu ya laki nne, smart phone, kaipata wapi? Nani kampa?
 
Back
Top Bottom