KERO Wazazi na Wanafunzi wa shule ya msingi Umoja, iliyopo Mabibo Farasi tunateseka kwa michango

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Viongozi wa mamlaka ya elimu wafanye ziara katika Shule ya Msingi Umoja iliyopo Mabibo Farasi, Kata ya Mabibo, Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam, na kuwahoji wanafunzi kuhusu michango ya shule ili kuona jinsi wazazi na watoto wanavyoteseka.

Kwa mfano, mzazi mwenye watoto wawili shuleni hapo hulipa takribani Sh18,000 au zaidi kila wiki. Endapo mzazi au mlezi hajampa mtoto fedha, mtoto huadhibiwa isivyo kawaida.

Binafsi, mwanangu anatakiwa kuwa na Sh500 ya mtihani kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi. Alhamisi anatakiwa kwenda na Sh1,500 kwa ajili ya mtihani wa wiki, pamoja na Sh1,000 ya chakula.

Serikali inasema elimu ni bure; bora warejeshe ada ili tujue, kwa kuwa wenye vipato vya chini wanaotegemea elimu bure ndio wanaoumia.
 
TULIPE KODI, ELIMU NI NGUMU KUWA BURE KWA NCHI MASIKINI, ELIMU BORA NI GHARAMA KWENYE HILI SIJUI TUNACHOMOKAJE CHOMOKAJE. .
 
Viongozi wa mamlaka ya elimu wafanye ziara katika Shule ya Msingi Umoja iliyopo Mabibo Farasi, Kata ya Mabibo, Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam, na kuwahoji wanafunzi kuhusu michango ya shule ili kuona jinsi wazazi na watoto wanavyoteseka.

Kwa mfano, mzazi mwenye watoto wawili shuleni hapo hulipa takribani Sh18,000 au zaidi kila wiki. Endapo mzazi au mlezi hajampa mtoto fedha, mtoto huadhibiwa isivyo kawaida.

Binafsi, mwanangu anatakiwa kuwa na Sh500 ya mtihani kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi. Alhamisi anatakiwa kwenda na Sh1,500 kwa ajili ya mtihani wa wiki, pamoja na Sh1,000 ya chakula.

Serikali inasema elimu ni bure; bora warejeshe ada ili tujue, kwa kuwa wenye vipato vya chini wanaotegemea elimu bure ndio wanaoumia.
Aisee! kila kona Nshale...
 
Ongeza na MBEZI INN SEC SCHOOL DARESALAAM.
watoto hawafundishwi vzr darasani wanalazimishwa kusoma tuition kwa mwezi ni sh 30000..
Tena no lazima..
 
Back
Top Bottom