Wazazi waeleza adha watoto 865 wakikikaa chini Mtambani Dar

Wazazi waeleza adha watoto 865 wakikikaa chini Mtambani Dar

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
photo_2025-06-07_20-04-55.jpg

DAR. Baadhi ya wazazi wa wanafunzi wanaosoma shule ya Msiungi Mtambani jijini Dar es Salaam, wameeleza adha ya watoto wao kukaa chini kwa kukosa madawati.

Dar es Salaam.

Kukosekana kwa madawati ya kutosha Shule ya Msingi Mtambani Bunju jijini hapa imefanya baadhi ya wanafunzi kusoma wakiwa wamekaa sakafuni jambo linaloathiri maendeleo yao ya elimu.
Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2002, hadi sasa ina wanafunzi 2,606 ikiwa na madawati 580 wakati mahitaji ni madawati 865 na hivyo kusababisha wananchi 867 kukaa chini.

Wakizungumza shueni hapo Juni 5, 2025 wakati wa sherehe za kupokea madawati 65 kutoka kwa kampuni ya ulinzi ya Gardaworld, baadhi ya wazazi wamesema hali hiyo inawapa wakati mgumu watoto wao kujifunza.
Anastazia Michael Mkazi wa Boko ambaye mtoto wake anasoma darasa nne shuleni hapo amesema amefurahishwa na msaada huo kwani kuna wakati wanatakiwa kuchangia madawati shuleni hapo.

"Tulikuwa tuna shida kubwa hapa shuleni, na madawati yalikuwa machache. Wanafunzi walikuwa wanakaa chini na wengine walikuwa wanashindwa hata kuandika vizuri. Lakini sasa, naona faraja kubwa kwa watoto wangu na wenzake. Sasa wana nafasi nzuri ya kujifunza, na wanafurahi zaidi," amesema Anastazia.

Jafari Abdallah ni mmoja wa wazazi aliyeshuhudia tukio hilo amesema endapo mtoto kama atasomea chini kukaa kwa kubanana lazima atakosa uhuru kusoma na kuandika vizuri, hivyo itampunguzia ufanisi darasani.
"Huu ni msaada mkubwa kwa watoto wetu na shule yetu kwa ujumla.

Madawati haya yatasaidia sana kupunguza kero za wanafunzi na walimu. Kila mtoto atakuwa na nafasi yake ya kujifunza kwa amani. Ni jambo la furaha kuona jamii inajitolea kusaidia shule zetu. Tunashukuru kwa moyo wa kusaidia," amesema Abdallah.

Dada mkuu wa shule hio anayesoma darasa la sita Gloria Nyamoko, kwa niaba ya wanafunzi wenzke wamehaidi kutunza madawati mapya waliopewa ili yatumike kwa muda mrefu.

"Tunashukuru kwa msaada huu wa madawati na kuhaidi kuyatunza ili kusaidia wanafunzi wa sasa na watakakaokuja siku za mbele. Kwani idadi hii ya madawati itakwenda kupunguza idadi ya wanafunzi waaokaa chini," amesema Gloria.

Akizungumza wakati wa kupokea madawati hayo, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Venance Mwasamakwela amesema kwa muda mrefu wanafunzi wamekuwa wakiketi chini au kushirikiana madawati kutokana na uhaba mkubwa wa samani hizo.

"Tunashukuru sana wahisani wetu sisi kama shule ya msimgi Mtambani kwa kuzawadiwa madawati 65 kutoka Gadaworld ambapo itapelekea kupunguza msongamano darasani kwenye ukaaji kwani wanafunzi 195 watakuwa wamepata pakukaa," amesema Mwasamakwela.

Mwasamakwela amesema msaada huo utakwenda kupunguza msongamano na kuongeza ari ya kujifunza kwa wanafunzi, huku akiahaidi kuyalinda madawati hayo ili yatumike kwa muda mrefu na mara baada ya msaada huo atakuwa na upungufu wa madawati 224.

Kwa upande wake, Kaimu Ofisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Kinondoni, Chitegese Dominic Ngaluku amesema Manispaa ya Kinondoni bado inauhitaji wa madawati, huku akiwata wadau kujitokeza kusaidia serikali katika kuchangia sekta ya elimu katika mahitaji mbalimbali.

“Ni jambo jema lilofanywa na wahisani wetu kwani tunapenda kuona kila mtoto anasoma katika mazingira rafiki na yenye staha. Hili ni jukumu letu sote kama jamii na sio kuiachia serikali pekee," amesema Chitegese.
Mkurugenzi wa kampuni ya Gardaworld, Goodluck Lukumani, amesema samani za darasani zinamchango mkubwa kwa wanafunzi kumsaidia katika masomo yake.

"Kushiriki kikamilifu kwa mwanafunzi akiwa darasani ni lazima apate mkao mzuri ndio maana sisi leo tumeamua kuwapatia madawati 65 ili yaende kupunguza pale kwenye shida. Tunaamini kwamba msaada huu utaleta matokeo chanya kwa wanafunzi na walimu kwa kuongeza ufaulu wao kwa ujumla," amesema Lukumani.
 
ni changamoto nayoamini itatatulika chini ya huyu mama wala sina shaka uzuri umelifikisha
 
Back
Top Bottom