Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Inadaiwa kulitokea gari ain ya Noah nyeusi ambayo haina namba iliyokuwa karibu na maeneo ya Shule, hali hiyo ikawashtua baadhi ya watu na kuanza kupeana taarifa juu ya uwepo wa gari hiyo ambayo baada ya muda iliondoka
Baada ya taarifa hiyo kusambaa Wazazi na Walezi wakakusanyika eneo la shule wakitaka kujua kama watoto wao wapo salama, wakazuiwa getini.
Idadi ilipoongezeka uongozi wa Shule ukaita Jeshi la Polisi kusaidia kuwatuliza Wazazi na Walezi, ambapo wakaanza kuwatoa Watoto, wakatumia Spika kuita majina ya Watoto kisha Mzazi au Mlezi anaingia ndani anathitishwa kama ndiye mwenye Mtoto anamchukua na kuondoka.
Watoto ambao hawakuwa na watu waliokuja kuwachukua wakalazimika kubaki Shuleni kwa muda