McCollum
JF-Expert Member
- Jan 10, 2023
- 384
- 684
Habari kwa wanajukwaa, ni matumaini Yangu muwazima wa afya. Tukiwa tunaelekea kuumaliza mwezi wa January napenda kulizungumzia suala la uelewa wa wahitimu wa darasa la Saba ambao kwasasa wako kidato cha kwanza.
Sitawazungumzia hao waliopita kwakuwa sina uzoefu nao, ila nataka kuwazungumzia hawa wanafunzi ambao walihitimu Elimu ya msingi mwaka 2022 ambao kwasasa wapo kidato cha kwanza. Nimekutana na wanafunzi zaidi ya watatu ambao nilipata wasaa wa kuwafundisha Hesabu, hali ilikuwa mbaya.
Scenario One: Mtoto wa kwanza aliniambi yeye mwalimu wake hajawahi kumfundisha kuhusu hizi symbols (< na >) na zingine zinazoshabiiana na hizo, nikaona linaweza likawa suala la usahaulifu, ila matatizo yakaanza kujionyeza baada ya huyo mwanafunzi kushindwa kuisoma 125,079 kwa Kiswahili aliishia kunitajia namba kimafungu akisema " 125 sifuri sabini na tisa" nikaona nitafute namna ya kumuelekeza lakini shida ikaja upande wa pili hata hesabu ndogo za hasi na chanya nazo zinamsumbua, kiufupi ni kwamba Hesabu kwake ni mtihani.
Scenario Two: Huyu mwingine yeye nilipojaribu kumuelekeza mada ya kwanza kabisa ya Hesabu naye alikuwa anapata shida hata kutambua kama namba ipo kwenye makumi, mamia au maelfu, na mara nyingi hata nilipomuandikia 10,000 nakumtaka aisome kwa Kiswahili naye alishindwa. Baada ya kumdadisi aliniambia alipata C ya hesabu na ana wastani wa B.
Conclusion: Wazazi/ walezi msiridhike na marks ambazo watoto wenu wanazipata kwenye mitihani hii ya Taifa mkizani inaakisi uwezo wao ki-Elimu, kama mzazi jipe hata muda wa ku"assess" uelewa wa mwanao, ukiona ana shida mahali tafuta namna ya kumsaidia. Hii mitihani ya ku"bet" inawapa wazazi matumaini ya bure kabisa.