Wazazi/ Walezi pambaneni na wahitimu wa darasa la saba, kwa bahati mbaya wengi wanauelewa usioridhisha

McCollum

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2023
Posts
384
Reaction score
684
Habari kwa wanajukwaa, ni matumaini Yangu muwazima wa afya. Tukiwa tunaelekea kuumaliza mwezi wa January napenda kulizungumzia suala la uelewa wa wahitimu wa darasa la Saba ambao kwasasa wako kidato cha kwanza.

Sitawazungumzia hao waliopita kwakuwa sina uzoefu nao, ila nataka kuwazungumzia hawa wanafunzi ambao walihitimu Elimu ya msingi mwaka 2022 ambao kwasasa wapo kidato cha kwanza. Nimekutana na wanafunzi zaidi ya watatu ambao nilipata wasaa wa kuwafundisha Hesabu, hali ilikuwa mbaya.

Scenario One: Mtoto wa kwanza aliniambi yeye mwalimu wake hajawahi kumfundisha kuhusu hizi symbols (< na >) na zingine zinazoshabiiana na hizo, nikaona linaweza likawa suala la usahaulifu, ila matatizo yakaanza kujionyeza baada ya huyo mwanafunzi kushindwa kuisoma 125,079 kwa Kiswahili aliishia kunitajia namba kimafungu akisema " 125 sifuri sabini na tisa" nikaona nitafute namna ya kumuelekeza lakini shida ikaja upande wa pili hata hesabu ndogo za hasi na chanya nazo zinamsumbua, kiufupi ni kwamba Hesabu kwake ni mtihani.

Scenario Two: Huyu mwingine yeye nilipojaribu kumuelekeza mada ya kwanza kabisa ya Hesabu naye alikuwa anapata shida hata kutambua kama namba ipo kwenye makumi, mamia au maelfu, na mara nyingi hata nilipomuandikia 10,000 nakumtaka aisome kwa Kiswahili naye alishindwa. Baada ya kumdadisi aliniambia alipata C ya hesabu na ana wastani wa B.

Conclusion: Wazazi/ walezi msiridhike na marks ambazo watoto wenu wanazipata kwenye mitihani hii ya Taifa mkizani inaakisi uwezo wao ki-Elimu, kama mzazi jipe hata muda wa ku"assess" uelewa wa mwanao, ukiona ana shida mahali tafuta namna ya kumsaidia. Hii mitihani ya ku"bet" inawapa wazazi matumaini ya bure kabisa.
 
na serikali pia iko responsible kwa kutoa elimu ya kukariri.
Ila kiukweli sikuwahi kuwaza kuwa tatizo linaweza kuwa kubwa kiasi hiki, hii mitihani ya ku"bet" itolewe tu. Huyo mwanafunzi wa pili aliniambia Mwalimu wao wa somo la Chemistry anaandika summary then anatoa maswali.

Hata baada ya kupitia daftari lake nilikutana na notes chache (hints tu) na Take Home Activities nyingi (Alikuja na daftari la Chemistry nimsaidie kumpatia majibu ya Importances tatu za Laboratory Rules, I felt the pain 😢)
 
Ila kiukweli sikuwahi kuwaza kuwa tatizo linaweza kuwa kubwa kiasi hiki, hii mitihani ya ku"bet" itolewe tu. Huyo mwanafunzi wa pili aliniambia Mwalimu wao wa somo la Chemistry anaandika summary then anatoa maswali.
Hata baada ya kupitia daftari lake nilikutana na notes chache (hints tu) na Take Home Activity nyingi (Alikuja na daftari la Chemistry nimsaidie kumpatia majibu ya Importances tatu za Laboratory Rules, I felt the pain 😢)
Mbaya zaidi huyo sio mmoja kuna mamilioni ya wenzie wanapita tuu shule tunazalisha taifa lenye mambumbu daily wasio kuwa na tija katika taifa.
 
Anita Makirita, kwa bahati mbaya hata shule anayosoma hii ni form one ya pili, form one ya kwanza ilianza mwaka jana.
Nchi yetu inahitaji major reforms kwenye swala la elimu, cha kushangaza viongozi wamelala fofofo sijui kwa nini wanashindwa kutumia platform kama hii JF kumake neccessary changes,ushauri mwingi unatolewa humu yaani ziiiiiiiii
 
Hizo >, < na nyingine watazisoma term ya pili kwenye numbers part 2.

Sio kila kichwa ni cha hesabu, wapo wanakamua namba vizuri sana hadi raha kuwavunjia mapindi.
 
Habari kwa wanajukwaa, ni matumaini Yangu muwazima wa afya. Tukiwa tunaelekea kuumaliza mwezi wa January napenda kulizungumzia suala la uelewa wa wahitimu wa darasa la Saba ambao kwasasa wako kidato cha kwanza.

Sitawazungumzia hao waliopita kwakuwa sina uzoefu nao, ila nataka kuwazungumzia hawa wanafunzi ambao walihitimu Elimu ya msingi mwaka 2022 ambao kwasasa wapo kidato cha kwanza. Nimekutana na wanafunzi zaidi ya watatu ambao nilipata wasaa wa kuwafundisha Hesabu, hali ilikuwa mbaya.

Scenario One: Mtoto wa kwanza aliniambi yeye mwalimu wake hajawahi kumfundisha kuhusu hizi symbols (< na >) na zingine zinazoshabiiana na hizo, nikaona linaweza likawa suala la usahaulifu, ila matatizo yakaanza kujionyeza baada ya huyo mwanafunzi kushindwa kuisoma 125,079 kwa Kiswahili aliishia kunitajia namba kimafungu akisema " 125 sifuri sabini na tisa" nikaona nitafute namna ya kumuelekeza lakini shida ikaja upande wa pili hata hesabu ndogo za hasi na chanya nazo zinamsumbua, kiufupi ni kwamba Hesabu kwake ni mtihani.

Scenario Two: Huyu mwingine yeye nilipojaribu kumuelekeza mada ya kwanza kabisa ya Hesabu naye alikuwa anapata shida hata kutambua kama namba ipo kwenye makumi, mamia au maelfu, na mara nyingi hata nilipomuandikia 10,000 nakumtaka aisome kwa Kiswahili naye alishindwa. Baada ya kumdadisi aliniambia alipata C ya hesabu na ana wastani wa B.

Conclusion: Wazazi/ walezi msiridhike na marks ambazo watoto wenu wanazipata kwenye mitihani hii ya Taifa mkizani inaakisi uwezo wao ki-Elimu, kama mzazi jipe hata muda wa ku"assess" uelewa wa mwanao, ukiona ana shida mahali tafuta namna ya kumsaidia. Hii mitihani ya ku"bet" inawapa wazazi matumaini ya bure kabisa.
Yani Mwanafunzi akitoka shallow shule ya msingi anakuwa mbumbumbu Bora kabisa kuwahi kutokea sekondari Yani anakuwa mgumu kwelikweli watu Huwa wanaangalia amefaulu la Saba basi mbona Bora huyo mwenye C je aliepata D Bora kumpigia mbuzi gitaa kuliko kumfundisha huyo Mwanafunzi ni adhabu nzito sana
 
Back
Top Bottom