Wazazi wanafiki hawafundishi IMANI vijana wao

Surya

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Posts
10,002
Reaction score
16,240
Huu ni ukweli usio pingika kuwa wazazi wengi hawapati Muda wa kuwafundisha vijana wao swala la imani, kwamba elimu ya shule, na Nyumba ya ibada ndio sehemu pekee tumejifunza tunayo yajua.

Na kibaya zaidi dini zote tulizonazo wabongo zinafundisha hasa, usifanye hichi ni dhambi fanya bidii kwenye mema tu.
Hilo ndilo wengi wanafata wakijua Mungu anaangalia hilo tu,
Na kumbe Kuhusu Imani ya kiroho hatujui chochote.

Mizimu hata kama kwenye familia ipo, kwanini watoto wasifundishwe kwa Maneno ya hekima,
Siku ya kupigwa Chale, unaambiwa tu twende kwa mganga bila kupewa maelezo.

Unakuta mzazi anaamini Mungu yupo, ila mtoto ni haamini kabisa, kwanini mzazi hafundishi Mwanae, ni siri au kutokujiamini ?
 
Kila mtu atabeba flushi lake! kama bado ni mdogo hapo wazazi wanakosea sana mkuu
 
Wasabato kwenye hili wanawapiga parefu sana watu wa dini zingine


Ni jukumu la mzazi kumfundisha mtoto Dini kwa wasabato
 
Watoto hawapaswi kuwa brainwashed kwa kufundishwa imana yoyote.
 
Malezi na mifumo ya maisha. Kwa ulimwengu wa leo hakuna conducive environment ya kumfanya mtoto awe karibu na imani ya Mungu. Inaonekana Kama old school
 
Watoto hawapaswi kuwa brainwashed kwa kufundishwa imana yoyote.
Unafikiri inawezekana kuishi bila Imani katika jambo fulani, ?

Kuamini kuwa kwenye familia yetu ni wanamuziki wakubwa ni Imani pia ya generation to generation na inaweza tengenezewa Mafundisho kama msingi wa kushikilia bila kuachia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…