Wazazi wanapaswa kupewa elimu ya njia za kumwadhibu mtoto kuepusha vifo na ulemavu

Wazazi wanapaswa kupewa elimu ya njia za kumwadhibu mtoto kuepusha vifo na ulemavu

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kuna haja wazazi na walezi kupewa elimu ya malezi ili kupunguza vifo vya watoto wao wanaowaua kwa kuwapa adhabu kubwa au hata ulemavu, kuwaachia makovu na majeraha moyoni kwa kuwapiga kupindukia wakiamini wanawaonya.

Matukio mengi ya wazazi na walezi kuwapiga watoto hadi kuwajeruhi zama hizi yameongezeka na inawezekana ni kutokana na baadhi yao kuwa na hasira, kukereka na hata kuchoshwa na mtoto anayotenda lakini pia wakikosa uelewa wa namna ya kulea hasa unapokasirika.

Katika matukio hayo ukitazama makosa, yanamhusu mtoto wa miaka minne kadokoa mboga au amevunja glasi au wakati mwingine kafanya kosa ambalo halistahili hata adhabu lakini mtoto anaadhibiwa hadi kufariki.

Ili kupunguza mikasa hiyo serikali na wadau wengine wafikirie namna ya kutoa elimu kwa wazazi na walezi hasa kuhusu malezi ya watoto ili kuwaongezea uelewa katika kujua namna bora ya kumdhibiti mtoto akifanya kosa kinyume na kipigo kikali kinachotolewa.

Au hata kama kosa lake linahitaji viboko wataelekezwa maeneo yapi ni sahihi kuwapiga ili yasitokee madhara ikiwamo kuwapa ulemavu au kuwaua.

Siku chache zilizopita tumeripoti matukio mengi wanayofanyiwa watoto na wazazi wanapoadhibiwa kitu ambacho kinabeba tafsiri kwamba yawezekana wengi wao hawana uelewa juu ya kuadhibu na kulea au wamechoshwa au kukerwa na mambo, hivyo kuhamishia hasira kwa watoto wao.

Ikumbukwe kuwa kumwadhibu mtoto si njia pekee ya kumfunza bali zipo nyingi za kutumia kumfundisha mtoto pale anapokuwa amekosea kinyume na kumwadhibu kupindukia.

Mtoto ni mtu anayekariri haraka zaidi kuliko mtu mzima hii ni kutokana na kutokuwa na mrundikano wa mambo mengi kichwani kwa hiyo akili yake hupokea na kupitia hali hiyo inawezekana akaelekezwa na akaelewa na kutii mapema.

Ni dhahiri kwamba taasisi nyingi za kiserikali na binafsi hazijaanza kufikiria upande wa pili wa sarafu kuwa wazazi na walezi wengine wana uelewa mdogo au wanatumia hasira zaidi kuadhibu watoto ili wajiandae kuwapatia elimu kama ilivyo kwenye mambo ya haki za watoto, ukatili wa kijinsia, semina za magonjwa, pamoja na masuala ya rushwa ya ngono ili kuhakikisha haki ya mtoto.

Hivyo kuna haja ya kuandaa mikakati na kulimaliza jambo hilo, ili kuipeleka elimu hiyo mbali hadi kupunguza vifo vya watoto vinavyotokana na kipigo cha wazazi pale wanapowaadhibu.

Kitendo cha mtoto aliyeadhibiwa na mama yake au mlezi kwa kudokoa dagaa na kuiba Sh. 250 hadi kufariki ni adhabu inayojaa fedheha na kuacha kovu kwenye familia.

Lakini katika kuchunguza inabainika kuwa hata wazazi ambao wamejikuta wakiingia kwenye kashfa ya kuua wakiadhibu watoto wao ni wale ambao walipata changamoto kwenye uzazi na huenda ni kupata watoto katika umri mdogo.

Hali iliyowasukuma kuingia katika majukumu bila kujua namna ya kuishi ndani ya majukumu hayo, mambo kama haya yameenea sehemu nyingi hali inayofananishwa na mtotto kulea mtoto mwenzake. Bila shaka katika muktadha huo siyo rahisi huyo mzazi kujua namna bora ya kutunza, kuadhibu na kufunza mwana.

Kivyovyote vile lazima itakuwa tofauti kwa hiyo ili kukikomboa kizazi kijacho kwa manufaa ya kutengeneza taifa bora na lenye watu waliokuzwa kwa usawa kuna haja ya kulibeba hili na kulifanyia kazi kikamilifu, serikali kwa maana ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii ikilipa uzito.

Pamoja kuandaa sheria na kanuni za kuadhibu wazazi na walezi wanaoadhibu kupindukia hata kuua tena kinyume cha sheria kwa vile wengi wao wanafanya bila kujua nini madhara ya baadaye.
 
Back
Top Bottom