Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
WAZAZI WAPUMZISHENI WATOTO WENU; NGOMA BADO NGUMU. WAPENI MOYO.
Anaandika, Robert Heriel
Inawezekana wewe ni miongoni mwa Vijana mnaopitia kipindi kigumu Kutokana na shinikizo la wazazi wakikutaka Uajiriwe.
Licha ya kuwaambia upatikanaji wa kazi umekuwa ni mgumu lakini bado wazazi wamekuwa wagumu kuelewa.
Wanakuona mzembe,
Wanakuona haujishughulishi,
Na imefikia hatua wanakuona hauna Faida, ni kama walipata hasara kukuzaa na kukusomesha.
Wanakuambia mbona wenzako wanapata ajira lakini wewe wanakuona umebung'aa. Lawama na mateto yamekuwa sehemu ya Maisha yako kila wakupigiapo simu. Inafikia hatua ukiona simu ya wazazi unaogopa kupokea.
Wazazi wapumzisheni Watoto wenu. Wapeni Moyo. Hali ni ngumu mno. Kuwasomesha Watoto wenu isiwe fimbo ya kuwachapia Watoto wenu. Jueni mnawapa hali ngumu huko walipo.
Mazingira yamebadilika Sana.
Elimu pekee haitoshi kumfanya mtoto wako afanye vizuri. Ni unyanyasaji, utendaji, uonevu kumshinikiza mtoto wako kuhusu mambo ya Kazi bila kuangalia mazingira ya dunia Hii yamekaaje.
Taikon mpaka naandika, nimekutana na visa na mikasa, nimejiridhisha Vijana wengi wapo katika Depression kubwa inayotokana na mashinikizo mengi ukiwepo shinikizo kutoka Kwa wazazi.
Wazazi msitake Watoto wenu wajiingize kwenye mishe hatari ili nao waonekane wanawatumieni Pesa.
Mnawaambia Watoto warudi nyumbani, wakirudi nyumbani shida, mnawasema, mnawanyanyasa, wengine wanafikia hatua ya kujiua, kujiingiza kwenye madawa ya kulevya.
Huku wengine wakiamua kuolewa ilimradi nao waondoke katika Himaya yenu.
Sio ajabu wengine wanapanga njama kuwaua ili warithi Mali.
Wakiondoka nyumbani Napo Kero.
Mtoto hajui atakula nini atakuwaza wewe?
Mtoto hajui atalipaje Kodi atakufikiria wewe? ATI kisa ulimsomesha?
Vijana wa sasa wanapitia kipindi kigumu mno. Wanahitaji Faraja, upendo, kuwaombea na sio kuwasema kisa wanashindwa kuwatumia Pesa.
Maneno yenu ya kejeli kisa ni wazazi hayafurahishi. Na kama Watoto wanashindwa kuwaambia, Mimi Taikon nitawaambia Ukweli. Mkiumia Sawa kwani hampendi ukweli, mkiukubali Sawa Pia.
Wapeni Watoto wenu mitaji, alafu wakishindwa kuwasaidia ndio mlalame na kuwakejeli, na sio muwatie Vijana Stress za kijinga jinga kisa mliwazaa au kuwasomesha. Hiyo sio Haki.
Nawapongeza wazazi wote wenye uelewa, wanaojua dunia Ipo kipindi gani. Waelimisheni wazazi wengine kuwa dunia ya sasa ni yakibepari, sio Ile dunia ya kijima tena.
Na ninyi wazazi mnaowapa Stress Watoto wenu acheni hiyo Tabia ya hovyo. Vijana wa sasa hatutavumilia.
Mnasema Vijana wa sasa wanalaana, laana mliwapa nyie sio?
Ninyi msio na laana mbona mnawasumbua wenye Laana badala ya kuwabariki?
Wapeni Moyo Watoto wenu. Maneno yenu ya kijinga na vitisho ni upuuzi tuu, mnaharibu jamii na taifa Kwa sababu ya ubinafsi wenu. Hamuvai viatu vya Watoto wenu ndio maana wanawatesa.
Badilikeni!
Nafahamu hata Mimi ni mzazi. Hivyo ujumbe huu unamhusu MTU yeyote.
Nipumzike SASA!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam