Wazazi wetu:-Mgeni akiwa anakula ukimuangalia unapigwa, ukipigwa ukalia unapigwa na usipolia unapigwa

Wazazi wetu:-Mgeni akiwa anakula ukimuangalia unapigwa, ukipigwa ukalia unapigwa na usipolia unapigwa

Unasema tu mkuu..
Nakumbuka wakati niko primary nilianguka kwenye bembea shuleni nikavunjika mkono na hapo nyumbani mzee alikua ananiambia kila siku nisibembee bembea za shuleni ni mbovu sikuskia.. Alivyopigiwa simu akaja kabla ya kufanya chochote akachukua kamba akanifunga mkono usioumia kwenye chuma la bembea nikawa naning'inia alinichapa vibaya mno[emoji24][emoji24][emoji24]..
Halafu ndo akanifungua tukaenda hospitali, ile siku nilichekwa sitakaa nisahau [emoji23][emoji23][emoji23]
Mbona kipindi hicho simu zilizokuwepo ni za mezani? Shule za primary hazikuwa na simu.
 
Mbona kipindi hicho simu zilizokuwepo ni za mezani? Shule za primary hazikuwa na simu.
sio wote tumezaliwa miaka ya 90 au themanini mkuuh😂😂.. primary nimemaliza 201…, Au basi kuna watu wangu wa maaana humu🤒🤒
 
Nakumbuka kulikuwa na redio, wakati wa taarifa ya habari ukisikika ukiongea unalo...

Unapigwa kibao Cha kimataifa, ukilia unapigwa Tena lingine nyamazaaaa..

Kwakweli tulipigika...
 
Unasema tu mkuu..
Nakumbuka wakati niko primary nilianguka kwenye bembea shuleni nikavunjika mkono na hapo nyumbani mzee alikua ananiambia kila siku nisibembee bembea za shuleni ni mbovu sikuskia.. Alivyopigiwa simu akaja kabla ya kufanya chochote akachukua kamba akanifunga mkono usioumia kwenye chuma la bembea nikawa naning'inia alinichapa vibaya mno😭😭😭..
Halafu ndo akanifungua tukaenda hospitali, ile siku nilichekwa sitakaa nisahau 😂😂😂
Mzee wako ako na ujasiri wa hali yajuu, nayaelewa maumivu ya kuvunjika mkono ni makali mno.

Mimi nilikua napigiwa kelele na mama kuhusu mpira, haipiti wiki sijaumia mpirani, mama yangu ni mpole sana ila ni mkali, huwa havumilii kitu anachoona sio sawa. Akawa ananiambia siku ukivunjika huko kwenye mampira yako utajitibu mwenyewe, maneno yake yakatimia nikavunjika mkono mpirani nadhani nilikuwa form 3/4.

Nilirudi nyumban kimya nikalala sikumwambia mtu nikiogopa mama kujua, imagine mkono umevunjika nikalala nao hivyo hivyo mpaka kesho yake nikatafuta bima asubuhi na mapema nikaenda hospitali ni mbali ila hata sikuomba nauli, nilifika nikakuta bado wanafanya usafi nikasubirishwa wakamaliza nikahudumiwa.

Baadae nmerudi nyumbani kila mtu anashtuka nipo na limhogo. Yale maumivu niliyoyapata ule usiku yalinifanya niachane jumla na kucheza mpira.
 
Back
Top Bottom