Wazee anayejua mganga mzuri, nimeibiwa tofali zangu site

NENDA MALAWI.
 
Mkuu, miezi 5 tofari zimekaa tu hii mbwinu ya wapi ya ujenzi.

Acha wenye haraka na ujenzi wazitumie.

Next time, tofali inafika site na kuanza kutumiwa.

Achana na waganga, umechangia ujenzi wa Taifa 🤣🤣
Wamemuotea tu mkuu 🤣, labda majirani zake hauongei nao vizuri.
Saiti tofali zinakata mpaka miaka 5, itakuwa miezi 5
 
Ukweli mchungu huu 🤣
 
Utaliwa pesa tu mzee hakuna waganga siamini katika hizi vitu, na utapata hasara zaidi, bora hiyo pesa ya kutafuta waganga ufanyie mambo mengine tu.
 
Hii itakuwa kazi ya Mpwanyungu maana amepotea sana siku hizi🤣🤣😀😀. Pole sana mkuu. Jipange upya. Achana na waganga watakula zaidi ya tofali.
 
Ukinunua tofali unatakiwa uliweke na cement sio kuliweka chini
 
Unatafuta mtu wa kukuibia mara ya pili?
 
Waganga ni matapeli hawana nguvu wala uwezo wowote, utapoteza tofali na pesa zako pia
 
Umenikumbusha 2007 konda wa hiace jijini Mwanza naye waling'oa grills za madirisha kwenye boma lake ambalo halijakamilika akawa anaulizia mganga kwa abiria!😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…