Wazee wa baraza wasema 'Lulu' ameua bila kukusudia, Jaji kutoa hukumu Novemba 13

Wazee wa baraza wasema 'Lulu' ameua bila kukusudia, Jaji kutoa hukumu Novemba 13

Atahukumiwa kifungo cha nje mwaka mmoja akiwa anafanya usafi stendi ya Ubungo
 
Pole Lulu; Hao wazee wamamkuta na hatia ya hili;

Manslaughter- 195. Any person who by an unlawful act or omission causes the death of another person is guilty of the felony termed "manslaughter" An unlawful omission is an omission amounting to culpable negligence to discharge a duty tending to the preservation of life or health, whether such omission is or is not accompanied by an intention to cause death or bodily harm.

Unatakiwa Kupambana ili uepuke hili;

Any person who commits the felony of manslaughter is liable to imprisonment for life.
Dogo ndio anapotea hivyo ile kamekula bata,sterehe mnazipenda ila mwisho wake mbaya
 
Pamoja na hayo yote lakini lazima tukubali kuna doa kubwa limeingia kwa mahakama na kwa mawakili wa serikali....ambalo hadi leo nashindwa kuelewa kama yule wakili wa serikali aliye kuwepo jana kama anazo akili timamu kweli au alilewa rushwa aliyopewa...
Kitendo cha kukubali ushahidi wa kijinga wa mke wa Dr Slaa kwakweli ni aibu kubwa kwa mahakama....
Kwakweli sidhani kama hukumu itaaminika kabisa...
Lulu atapewa kifungo cha nje hakuna jipya..............
Mke wa Dr Slaa ni Daktari? Kosa la kuua bila kukusudia ni kifungo cha nje?
 
Ataachia huru huyu ,sheria dunia haki mbinguni ,angekua sio MTU maarufu angepigwa mvua za kutosha ila huyu ni superstar na si mnajua mahakama za bongo ni za wanyonge tu ndo zinawatupa jela tena miaka mingi kwa makosa ya kijinga kabisa
Nimeipenda hii,sure kabisa wanyonge ndio wanaozea jela wengine bila hata hatia
 
Ukihangaika saaana mwisho unapata matatizo,Nina wasi wasi aliambiwa sana na wazazi wake lakini hakusikia.Mungu amfanyie wepesi katika jambo hili,ni zito hasa ukijiweka kwenye viatu vyake.Ana wakati mgumu saana.Mimi si mpenzi sana wa mambo yake lakini amekabiliwa na tatizo kubwa inabidi kama binadamu tumuhurumie na kumuombea.
 
"Muuaji" albeit bila kukusudia anakaaje nje "kwa dhamana"? Akiua tena na tena?
 
Maamuzi ya kesi hii yanaweza kufanana na ilivyokuwa kesi Ya Chenge..Ila itategemea na upande wa Family ya Kanumba..
 
Waungwana
Mmesahau ya Mtemi Chenge
Aliua wanawake wawili kama sikosei kwa kuwagonga na gari

Alitiwa hatiani kuua bila kukusudia
Alipewa adhabu ya faini Laki 7

The rest is history

Leo anaendelea kuwa Mbunge na Mwenyekiti wa Bunge

Pia ndio Mwandishi wa Katiba Pendekezwa iliyopitishwa na Bunge la Katiba
Kesi yake ni tofauti na ya huyu...hiyo ya chenge ilikuwa ni traffic case,sio ordinary crime kama zile za kwenye Kanuni ya Adhabu (Penal Code)
 
Inaonekana una upeo mzuri wa kisheria, je unaweza kunisaidia ni kwa nini kesi ya Lulu haijaendeshwa kwenye Juvenile court hasa ukizingatia alikamatwa akiwa under 18 years old?
Naweza kusaidia pia.

Si kila kosa analotenda mtoto litasikilizwa juvenile/children court...kuna baadhi ya specified offences hata kama aliyetenda ni mtoto basi atashitkiwa katika mahakama za kawaida...Miongoni mwa makosa hayo ni kama vile Murder/Manslaughter, Rape nk.

Hapo tunazungumzia under 18 with exception to boy below 12 yrs ambao they are presumed kuwa hawawezi kutenda sexual offences...and below 10 yrs who are presumed cannot commit any offence at all..hii ni kutokana na kwamba hawana uwezo wa kuform intention.

Stand to be corrected,if kuna sehemu nimeteleza kidogo.
 
Back
Top Bottom