Mnachihanguuu
JF-Expert Member
- Feb 10, 2023
- 6,406
- 9,830
Kaka watu wana pesa hivi ni vitu vya kawaida sana umaskini ni kitu kibaya mno kila kitu unaona hakiwezekani...hivi nikikuambia Kuna dogo alisuka mkeka wa mechi 8 akaweka elfu 15 na ndani ya mkeka huo iĺikuwepo mechi ya yanga vs tabora na chakushangaza alimuua Yanga utaamini? Kama ungekuwepo hapa mjini mtwara kijiwe cha sweet corner ungeulizia ni nani aliweka sare kwenye game ya Tanzania na Tunisia ungeonyeshwa huyo mshkajiiNgooo
Mimi naona kila kitu ni kamali tu fikiria wewe wazazi wako walikomaa kukusomesha ili upate ajira mwishoni hauna kazi...mwaka jana nilikuwepo kwenye timu ya mgombea ubunge mmoja kwenye mchakato wa kura za maoni za ccm jimbo la newala mjini,Jina la huyo jamaa halikuwa maarufu hata kidogo ila usiku wa mwisho kabla ya kura za maoni tulimwaga pesa kila mjumbe akila 20000 fikiria wajumbe wa jimbo zima wote wapate pesa hiyo...tukafika kijiji cha chiwhindi ambako ni kwao mbunge wa sasa nako ikamwagwa pesa mpaka kwa timu ya mpinzani wetuAnahamasisha betting, hata kusuka mkeka hajui
Bado nikiwango himilifu siku akipigwa 20M hapo nitamsikitikiaLeo amepigwa tena pesa mingiView attachment 3531618
Ndo maana anuza mikeka buku mbili mbili! Yaani nikanunue kabisa mkeka odds 1.8!Bado nikiwango himilifu siku akipigwa 20M hapo nitamsikitikia
Kampuni gani lina laghai wa hivo?Kamari ya betting ni tofauti na hizo scam ambazo mnaziongelea.
Betting ya mpira sio biko wala tatu mzuka kuwa wahusika wenyewe ndio wanaojua ukweli wa matokeo.
Naweza kusema Betting ya mpira ndio kamari yenye uwazi kuliko kamari nyingine.
Labda hapa useme baadhi ya makampuni ambayo yamekuwa yanahusishwa na tuhuma za ulaghai kama kufuta slips endapo uta win pesa nyingi.
Lakini kusema sijui wakina fulani na fulani wanatumiwa na makampuni kutoa mikeka ili kuwaingiza chaka wengine, sio kweli.