Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 53,537
- 133,017
Kwanza inaonekana hata maana ya biashara huijui.Unajua maana biashara? Mwenye biashara ya betting ni mmiliki wa kampuni yeye habashiri anafanya biashara. Wewe ndiye unayebashiri , ndio maana siku zote unaambiwa beti kwa kiasi unachomudu kupoteza.
Biashara ni shughuli yeyote ya kubadilishana thamani kwa lengo la kupata faida.
Mmiliki wa kampuni ya betting anafanya biashara kwa kuuza odds na huduma ya kubashiri.
Lakini mteja anayebeti pia anafanya biashara anawekeza mtaji wake (stake) kwa matarajio ya faida (payout). Hii ni biashara ya ubashiri, sawa na mtu anayewekeza kwenye soko la hisa au forex.
Mmiliki wa kampuni naye ni mbashiri kwa maana ya risk management anaweka odds kwa matarajio kwamba wateja wengi watapoteza. Huu ni ubashiri pia na ndio maana analiwa vile vile.
Kama mmiliki hafanyi ubashiri, kwa nini odds hubadilika kulingana na form ya timu au idadi ya watu walioweka beti?
Kama mteja si mfanyabiashara, kwa nini betting inaitwa “stake” (uwekezaji wa mtaji) na “payout” (faida)?