Wazee wa Betting mmeona mwenzenu Hanscana ameliwa Milioni 7.5?

Wazee wa Betting mmeona mwenzenu Hanscana ameliwa Milioni 7.5?

Huyu dogo anaya chezea MAISHA SI Bora ange FANYA biashara HUWEZI ishi KWA kutegemea kamali
Sasa unasema anachezea maisha huku unakuta yuko kwenye payroll ya 10M per month.

Huenda ana mkataba wa hata 300M kwa miaka 3 ku promote kampuni za kamari tofauti tofauti!
 
Sasa unasema anachezea maisha huku unakuta yuko kwenye payroll ya 10M per month.

Huenda ana mkataba wa hata 300M kwa miaka 3 ku promote kampuni za kamari tofauti tofauti!
Na hata ukiona mtu amapeteza fedha kubwa asilimia kubwa amewahi kushinda kiasi kikubwa , pia kuna urahisi fulani wakupata hiyo pesa tofauti na mtu mwingine huwezi kubeba tofali alafu uje ubeti milion 7 kwa mara moja no.
 
Yeah.

Ni kama wale matapeli wa kwenye stendi za mabasi hasa pale Magufuli Mbezi Luis.

Unakuta kimekaa kikundi cha watu, kinazungusha vikadi, vya bahati nasibu, kumbe wote ni group moja. Mtu akijichanganya akaenda hapo, analiwa mchana kweupe.
Walinila elfu 2 yangu wakati wa Ubungo Terminal😆
 
Sasa kama wapo ndani ya limit watazuiwa vipi? Nimekwambia risk ya kampuni kupata hasara inazuiwa kwa mtu mmoja mmoja kwasababu haiwezekani kila mtu kushinda lakinI inawezekana mtu mmoja kushinda kiasi kikubwa
Ni kweli hata mimi sijapinga hilo sijui kama unanielewa.

Nachopinga mimi ni hiki

Kusema kwamba hata ukibeti ukashinda hautalipwa. Hii napinga kwasababu mpaka bet inafanikiwa kuruhusiwa maana yake mifumo imekagua na kuona payout iko ndani ya uwezo wa kampuni.

Hakuna namna ambayo kampuni litakuwa na uhalali wa kisheria kutolipa bet kwa mshindi kisa amevuka kiwango.

Kingine ambacho najaribu kukuelezea ni kwamba.

Kampuni kusema kiwango chao cha mwisho kumlipa mtu mmoja ni milioni 500 haina maana kwamba ikitokea watu tofauti tofauti wameshinda bet zao wengine milioni 10, wengine laki na total amount ya pesa ni bilioni 1 hawawezi kulipwa.

Lazima walipwe.

Mimi huku kwenye dashboard ya mkeka itasoma nimeshinda elfu hamsini haitasoma ujumbe kuwa "wewe na wenzako 1,000 kutoka pande tofauti tofauti duniani kwa jumla wenu mmeshinda pesa zaidi ya bilioni 1 ambayo ipo nje ya uwezo wetu na hivyo hatuwezi kuwalipa"
 
haiwezekani kila mtu kushinda lakinI inawezekana mtu mmoja kushinda kiasi kikubwa
Ni kweli haiwezekani kila mtu kushinda

Lakini pia kuna kipindi ambacho timu zinatoa magoli na kufungana sana, hiki kipindi watu wengi hushinda bet zao.

Kwa hiyo hata kama kuna idadi ya watu wanaopoteza bado kuna sehemu ambayo kampuni inaweza kupata pigo ikiwa mechi nyingi zikaenda vizuri.

Na pia ukumbuke kuna watu wanao stake high, hao watu bet zao zikishinda kama kampuni inajitafuta inaweza kufilisika.
 
Kumbe watu wanapiga pesa ndefu hivi, nipo nasoma kila comment kwenye huu Uzi mwaka huu lazima nijifunze kubeti
 
Acha upotoshaji. Ukiona mkeka wako umefutwa ujue kuna fraud umefanya , na hii hushughulikiwa kwenye risk management. Unaweza kuokota fixed game ukaiweka kwenye mkeka wako unadhani utalipwa? Ticket inafutwa na unaweza kufutiwa account . Halafu wasafi bet suo kampuni ndogo nimiongoni mwa kampuni 10 zenye mtaji mkubwa afrika mashariki. Kampuni hii inamilikiwa na matajirI wa Belarus ambao wanamiliki pia Oddbet kenya ambapo walifanya partnership na diamond kuingia kwenye market ya Tanzania
Fraud kwenye mkeka inafanywaje?

Na je mechi hiyo itakuwa ni fraud kwa watu wote walioifuata au ni kwangu tu?

Mbona umeibua kitu kipya ambacho ni more controversial?

Fixed game inawezaje kuwekwa kwenye fixtures za betting?

Yani kampuni linajua kwamba mechi hii ni fixing lakini bado likaamua kuiweka kwenye market, hiyo mechi ili baadaye mtu akibeti mkeka ufutwe na pesa asilipwe kwa madai ya fraud?
 
Tutajie kampuni iliyofilisika kwa ushindi wa wateja mkuu
Kampuni likifilisika halisemi tumefikisika

LBL walivyo tapeli watu hawakusema kuwa tumewatapeli.

Kufilisika kwa kampuni kupitia ushindi wa wateja tunaupima kwa factors za malipo kucheleweshwa siku ambayo bet nyingi za watu zilishinda.

Na baada ya hapo ndio ikawa mwisho wa kampuni kuendelea kufanya shughuli za betting.

Haiwezi kuwa coincidence kwamba siku ambayo watu wameshinda kwa wingi ndio kampuni likapata matatizo ya mtandao, kampuni likabania pesa za watu, halafu mwishowe likatangaza kusitisha huduma zake.
 
Nimekupa mtazamo wa chatgpt , kampuni itafiliska kwa mambo mengine lakini sio kwasababu wateja wameshinda kwasababu kiwango cha ushindi kina limit , hamuwezi kushinda zaidi ya mtaji wa kampuni. Na kampuni zinatofautiana kwenye limit , nyingi hauwezi kushinda zaid ya milion 500 , nikakupa mfano kampuni 1 tajiri duniani kwenye betting unaweza kushinda hadi trilion 1000 ila timu hazitakiwi kuwa zaidi ya 50 na siku ukishinda utalipwa pesa yako na utaona Kampuni ikiendelea na watafurahia ushindi wako kwasababu utawatangaza zaidi. Na kuna uwezekano ukawarudishia sehemu ya hiyo pesa kwa kupoteza kama ukiendelea kubeti
Sasa Kampuni ya betting shughuli zake ni betting kati ya kupuna au kupunwa, inafilisikaje bila kuhusisha kuliwa?

Wewe kuna mambo mengi huyajui na unakomaa kubisha.

Betting ni ubashiri, kama ambavyo mimi naweka mategemeo kuwa nitashinda naye mmiliki wa kampuni anakuwa na mategemeo hayo hayo.

Hakuna limitation ya watu kubet kisa tu idadi ya mikeka iliyowekwa imezidi mtaji wa kampuni.

Na ndio maana huwezi kusikia kampuni fulani leo limejaa haliruhusu watu wapya kubeti kwasababu waliobeti wameweka mikeka yenye payout kubwa kufikia mtaji wa kampuni.

Watu wataendelea kubeti tu kwasababu kampuni linakuwa na matarajio kwamba watu watapoteza na yeye ndio faida yake.

Sasa ikitokea watu wamekula kulIko mtaji wake ni lazima hizo pesa zilipwe, hii kazi ina hasara pia.

Hakuna biashara isyokuwa na hasara japo inaweza kuonekana ni hasara ya muda mfupi lakini bado ni hasara.
 
Kwamba kujua hawana demo account hiyo nayo mpaka iwe na hisa?
Mfano wewe unajua crdb wana huduma ya simbanking, je kwa kujua hilo maana yake wewe una hisa crdb?
Kwani njia ya PR ni moja tu? Kwani wakimpa kibunda cash awe anabet wewe utajuaje? Kwani nao unazan ni wajinga, kama hadi wewe hapo manzese unajua watu wa demo account ni matapeli bas nawao wanakuja kivingne ili waendelee kuneemeka
 
Sasa Kampuni ya betting shughuli zake ni betting kati ya kupuna au kupunwa, inafilisikaje bila kuhusisha kuliwa?

Wewe kuna mambo mengi huyajui na unakomaa kubisha.

Betting ni ubashiri, kama ambavyo mimi naweka mategemeo kuwa nitashinda naye mmiliki wa kampuni anakuwa na mategemeo hayo hayo.

Hakuna limitation ya watu kubet kisa tu idadi ya mikeka iliyowekwa imezidi mtaji wa kampuni.

Na ndio maana huwezi kusikia kampuni fulani leo limejaa haliruhusu watu wapya kubeti kwasababu waliobeti wameweka mikeka yenye payout kubwa kufikia mtaji wa kampuni.

Watu wataendelea kubeti tu kwasababu kampuni linakuwa na matarajio kwamba watu watapoteza na yeye ndio faida yake.

Sasa ikitokea watu wamekula kulIko mtaji wake ni lazima hizo pesa zilipwe, hii kazi ina hasara pia.

Hakuna biashara isyokuwa na hasara japo inaweza kuonekana ni hasara ya muda mfupi lakini bado ni hasara.
Unajua maana biashara? Mwenye biashara ya betting ni mmiliki wa kampuni yeye habashiri anafanya biashara. Wewe ndiye unayebashiri , ndio maana siku zote unaambiwa beti kwa kiasi unachomudu kupoteza.
 
Kampuni likifilisika halisemi tumefikisika

LBL walivyo tapeli watu hawakusema kuwa tumewatapeli.

Kufilisika kwa kampuni kupitia ushindi wa wateja tunaupima kwa factors za malipo kucheleweshwa siku ambayo bet nyingi za watu zilishinda.

Na baada ya hapo ndio ikawa mwisho wa kampuni kuendelea kufanya shughuli za betting.

Haiwezi kuwa coincidence kwamba siku ambayo watu wameshinda kwa wingi ndio kampuni likapata matatizo ya mtandao, kampuni likabania pesa za watu, halafu mwishowe likatangaza kusitisha huduma zake.
LBL sio kampuni ya betting mkuu ni matapeli kama mfano wako ndio huo bora mjadala tuufunge
 
Fraud kwenye mkeka inafanywaje?

Na je mechi hiyo itakuwa ni fraud kwa watu wote walioifuata au ni kwangu tu?

Mbona umeibua kitu kipya ambacho ni more controversial?

Fixed game inawezaje kuwekwa kwenye fixtures za betting?

Yani kampuni linajua kwamba mechi hii ni fixing lakini bado likaamua kuiweka kwenye market, hiyo mechi ili baadaye mtu akibeti mkeka ufutwe na pesa asilipwe kwa madai ya fraud?
Fixed game maana yake ni mchezo uliopangwa matokeo, kwenye system zao kuna tabia zikifanyika ambazo sio za kawaida ina detect kama ni fixed game. , kampuni za kubashiri hazimiliki vitabu vya betting na odds huwa wananunua kama ilivyo kutoka katika kampuni zinazotengeneza vitabu vya betting kwahiyo kama fraud imefanyika kwa mteja maana yake wenye kukumu la kujua ni kampuni husika gemu husika inafungwa odds au mteja aliteshinda halipwi. Fixed game sio prediction ni mchezo ulionunuliwa moja kwa moja .
 
Ni kweli haiwezekani kila mtu kushinda

Lakini pia kuna kipindi ambacho timu zinatoa magoli na kufungana sana, hiki kipindi watu wengi hushinda bet zao.

Kwa hiyo hata kama kuna idadi ya watu wanaopoteza bado kuna sehemu ambayo kampuni inaweza kupata pigo ikiwa mechi nyingi zikaenda vizuri.

Na pia ukumbuke kuna watu wanao stake high, hao watu bet zao zikishinda kama kampuni inajitafuta inaweza kufilisika.
Bado kiwango wanachoshinda hakiwezi kuwa pigo kwenye kampuni ya betting kijana wewe kwenye maisha yako kuacha jackpot ya sport pesa umewahi kusikia hata mtu ameshinda bilion kwenye betting? Kushinda pesa nyingi kwenye betting sio jambo linaloweza kutokea kirahisi ndio mana nimesema kampuni ya betting kufilisika kwasababu ya ushindI nijambo ambalo haliwezekani kwasababu kwanza wana njia nyingi za kulinda mtaji wao ikiwa ni pamoja na limit ya ushind kwa kila mteja
 
Pia silimia kubwa ya watu wanaoshinda betting ni either alishawahi kupoteza kiasi kikubwa kuliko alichoshinda au kiasi alichoshinda kuna uwezekano aka kirudisha chote na ziada. Sasa biashara ya namna hiyo utaifilisije.
Nasio kwamba wanaweka mtaji wanatulia kuna idara za hesabu ambazo kwanza wanaweza kugundua hata uwezekano wa tickets yako kushinda , ndio mana unaona mambo kama cashout kazi yao nikufanya analyss kwa jinsi mchezo unavyokwenda , kiasi kwamba wanaweza kutawanya hasara . Mwanzoni nilikwambia ukiacha madawa ya kulevya na biashara ya filam za ngono biashara namba 3 kwa kuingiza mkwanja ni igaming
 
Back
Top Bottom