Hiyo ya PSG win either half bado ni option ngumu...kwa mtazamo Wangu walau angeomba goli moja kwa mechi nzima.
Haipo hivyo sasa.
Tambua kuwa siku zote odds zinaundwa kumlinda mwenye kampuni kuliko wewe mteja (Mkamaria)
Kwa hiyo kwenye mechi ambayo kila mtu anajua intensity ya competition ni 60% dhidi ya 40% maana yake watu wote wataobeti mechi hii ili wawe salama lazima wamfuate huyo mwenye 60%
Na hapo ndio kampuni litaweka odds chache kwa huyo mwenye 60% ili hata ikitokea ameshinda basi haupati hela nyingi.
Hapo ndio watu wanaona bora waweke pesa nyingi ili wakibeti mechi hiyo wapate hela nzuri.
Sasa mechi ya jana ilikuwa ni 90% dhidi ya 10%. Ni nani ambaye angeweza kuthubutu kumbetia huyu wa 10% ambaye kapanda ligi msimu huu halafu aje amfunge bingwa wa muda wote wa Ligi 1 na Bingwa mtetezi wa UEFA?
Kwa hiyo kwa factors hizo muhindi anapanga odds ndogo.
Wewe unasema bora angeweka goli 1 lakini mechi ya jana odds za magoli zilianzia magoli mawili.
Option ya kubeti goli 1 kwa jumla ya mechi lipatikane haikuwepo, kwasababu ni odds ambayo ilionekana kuwa ni nyepesi mno.
Na kama ingekuwepo si ajabu ingepatiwa odds ya 1.01 yaani weka stake ya laki ili upate laki na buku. Sasa nani angeweza kuthubutu kufanya huo uchale?
Ila sasa angeweka goli moja lipatikane kwa Paris kama ilivyotokea, si ajabu odds zilikuwa zaidi ya 6. Lakini swali ni je, ni nani angeweza kuchukua risk kuibetia timu ambayo makadirio ya chini ilikuwa ni goli 4 bila?