mana sex ni hitaji la muhim ila ili isiwe dhambi ni bora ukafanya tendo la ndoa katika ndoa kuliko kuzini(kama unataka kutengeneza mahusiano yako na Mungu mana dhambi inakutenga na Mungu)
Tendo la ndoa ni muhimu kwenye ndoa ila sio sababu pekee,sababu nyingine haikumpendeza Mungu mwanaume aliyemuumba aishi peke yake akamfanyia na msaidizi wa KUFANANA NAYE akamfanyia mwanamke ambaye Adamu alimuona kuwa ni SAHIHI kwake akamuita nyama katika nyama yake mfupa katika mfupa wake.
Ukipata mwenza sahihi kutoka kwa Mungu ndiye anauwezo wa kukupatia mke sahihi kwako,mke sahihi kwa mwingine anaweza asiwe sahihi kwako.
Kupata watoto na mengineyo hayo ni matunda baraka na neema za Mungu.
KWELI KUNA WAPO WANAOPATA WENZA WASIO SAHIHI hawa ndio wanaochukia ndoa kwa sababu ya uzoefu mbaya waliopitia katika mahusiano yao.Lakini mahusiano yako siyo ya mwingine ndoa zetu hazifanani,uzoefu wako hauwezi kutumika kushauri ama kuamua ndoa za wengine wote.ILA ukimuomba Mungu wenza wema na sahihi wapo,
Kama mimi Mungu amenipa mke mwema na sahihi na ndoa yenye amani furahabna upendo,na umoja nafurahia ndoa yangu.Naamini hata wengine Mungu anaweza kuwapatia wenza sahihi kwao wa kufanana na kuendana nao.Tuwaombee wenza wetu kama ni sahihi na ndio Mungu aliotuchagulia basi Mungu atawabadilisha na sisi pia tusiwe chanzo cha kuwakosea wenza wetu tuwapende wake zetu kama Kristo alivyolipenda kanisa na kuombea nfoa zetu na familia zetu.Mungu atusaidie.