Wazee wa miaka ya 90, huu wimbo wa Shambani kutoka - RTD unakukumbusha wapi?

Wazee wa miaka ya 90, huu wimbo wa Shambani kutoka - RTD unakukumbusha wapi?


View: https://www.youtube.com/watch?v=_PCe60hMfms
Mimi unanikumbusha redio ya cassette ya panasonic mida ya menu mchana RTD nikiwa na mama na marehemu babangu.
Kweli muda unakimbia sana.
Mshana Jr

Enzi hizo kulikuwa na vipindi redioni ''MTU NI AFYA''
wakiimba wimbo'' kuleni chakula bora,mboga samaki maziwa...''
Haya mambo ndo tulitakiwa kuwauliza akina na mzee wetu wassirra watusimulie
siyo kila siku kushindana na vijana ambao mapafu yao bado yana uwezo wa kuhutubia masaa matatu non stop.
 
Huu wimbo ulikuwa ni sig tune ya kipindi cha Salaam Mkulima, kilikuwa ni kipindi cha salamu za wakulima, kinaanza saa 11:00 jioni mpaka 12:00 kwenye Idhaa ya Taifa, baada ya kipindi cha Karibu Vijana, Saa 10:15-11:00. Saa 10:00 kulikuwa na muhtaasari wa habari for 5min ikifuatiwa na matangazo ya Vifo hadi 10:15

Nikiwa Mtangazaji wa RTD, nimetangaza sana kipindi hiki!.
P
💪
 
Back
Top Bottom