Mizania
JF-Expert Member
- May 17, 2023
- 3,812
- 3,277
Mkuu;Na walishajiwekea utaratibu wa nafasi za benki kuu, TRA,maafsa kwenye balozi nchi za nje hauwezi kuona huko mtu wa kawaida lazma awe mtoto wa flan bin flan, JPM alipoingia akarudisha wote nchini akapeleka wengine watoto wa maskini ambao hawakuwazia kama ipo siku watafanya kazi kwenye ubalozi nchi za nje.
Kwanza tukubaliane kuwa watoto wa kiongozi, Tajiri na masikini wote ni raia wa Tanzania na wana haki ya kuajirika kwa kukidhi vigezo na masharti ya ajira.
Pili, sio kweli na sio vyema kugeneralize au kupotray kuwa nafasi zote kwenye taasisi ulizooredhesha zime hodhiwa kwa watoto wa kada ya viongozi, ushawishi na wenye ukwasi tu.
Tatu, ukichukulia kwa mfano TRA nchi nzima inaweza kuwa na wafanyakazi wasiopungua 3,000 ukiscrutinize watoto wa viongozi wanaweza was ifike hata 20, Avery minute percentage! Na wapo kwenye different level, and honestly waliobahatika wakafika top level wapo pale on merits!
Nne, tuache chuki na kujiona sisi ndio tuna haki zaidi kuliko wengine! Tuache kulia lia kila wakati na kuplay victims every time and then! Mlidanganyika kuwa nyie ni wanyonge! Hakuna mtanzania mnyonge wala masikini!
Tano, hata kwenye political class watoto wa viongozi ni wachache sana compared to the other classes, lakini utakuta mtu kapanua mdomo kupiga keleeeeele utafikiri mdomo wa kiboko!! Utafikiri watoto wa viongozi sio watanzania, au katiba imewakataza kushika nafasi yoyote nchini! wivu mtupu!
Sita, ili kila mtu afaidike, let's put the government of the day to task icreate more than enough jobs ili kila mtu aajirike, hizi kelele ndio zitaisha!
Lakini kama maandamano tu, jambo halali kikatiba inaonekana ni vurugu na nongwa! Kwanini mtoto wa kiongozi kuwa kwenye nafasi asitafsirike kuwa kapendelewa! Ujinga mtupu!
Mkuu, ajenda kuu ya uchaguzi iwe ni ajira! Tuache wivu na chuki!