Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Heri busara ilikuongoza kunyuti, kuna wanaojiaminigi kupitiliza na vyombo (haiwezi kaa hii mkali wa offroad), majuto huwa ni mjukuu.
Offroad nazikubali zaidi Landrover 110. Niliwahi kukuta mto umetema huko Manyara gari kibao zimepaki wanasubiri mto upungue.

Kufika pale kucheki maji hayana kasi, nikatia 4wD, Lock diff na Low range. Nikaingia nzima nzima chuma ikaogelea nikatoka upande wa pili.

Jamaa mmoja wa Landcruiser akaona kumbe simple tu nae akafata ila hakutoboa akakaa karibia na kutoka mwishoni.

Ilibidi nirudi tena humo humo kwa reverse nikasimama nikampiga belt na kumkokota hadi ng'ambo. [emoji1373][emoji1373]

Ukiachana na hilo tukio pia kuna sehemu nyingi sana nimewahi kuwakalisha wenye LC's tena kwenye tope ndio usiseme.

 
Asalaam, mrejesho wangu sio wa kulalama ila ni kujaribu ku draw attention ya politicians to do something, T1 yetu inahitaji msukumo hasa wa political will,tuijenge upya sio kuiwekea viraka, yule mkandarasi aliyejenga kile kilima cha kushukukia mikumi mjini aturudishie chenji yetu ule ujenzi ni zero, Iyovi pass not bad ile zile tutas loo, why tutas in the middle of nowhere?,Kitonga pass ni cancer level 4(mgonjwa anakufa sio kutibika),Chimala hadi Tunduma OSBP ni mbovu mno ,T2 kuanzia Nakonde hadi Isoka ni mix bag (inajengwa na ikiisha itakuwa super road),Isoka to Chinsali ni safi, na kati ya Chinsali to Serenje nayo ni mix bag,Ile bwawa la samaki limepigwa kifusi cha ovyo, na kutoka Serenje to kapiri ni safi,checks points za T1 hasa Sanga Sanga, Ruaha darajani ni pasta kichwa ,T2 zile za Chinsali, Mpika na Mkushi nazo ni Pasua kichwa, Dar to Moro ni lazima tufanye maarifa ya kupunguza traffic jam, like malori yapewe muda maalum wa kusafiri kwenye kipande hiki, thanks
 
[emoji1787] Tuko pamoja mkuu,hebu niambie nini kimejiri.
Driver mwenzetu alipata ajali pande za simiyu akiwa na Mark x nadhani umeona picha hilo limetrend kwenye page yetu ya road trip.

Mengine ni updates za wana wakiwa wanakiwasha bila kusahau mapicha picha ya natural vegetation ya nchi yetu mkuu.
 
Mwana unaninii na mods
Unajua humu ndani kuna baadhi ya members wanazingua kinyama. Mfano kuna uzi jamaa anauza Raum yeye anaita Raum new model ni ya mwaka 2004[emoji848]

Sasa yule bwana nilikuwa najibizana nae sana, majibizano yalianza baada ya yeye kuambiwa hiyo sio new model. Akaambiwa kama hiyo ya 2004 unaita new model vipi ya 2015/2017

Jamaa alijaa sumu hatari akaishia kuporomosha lugha ngumu, kuna dhana humu ndani ya kumwita mtu dada ilihali sio, sasa yeye akawa anatumia hiyo lugha kama ngao.

Mimi wala sikumjibu shi.t, sasa raia kama hawa ukienda naye jino kwa jino ukashindwa kudhibiti emotion aisee ban inaweza kukuhusu.
 
Niliwaona 😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…