Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Asalaam, mrejesho wangu sio wa kulalama ila ni kujaribu ku draw attention ya politicians to do something, T1 yetu inahitaji msukumo hasa wa political will,tuijenge upya sio kuiwekea viraka, yule mkandarasi aliyejenga kile kilima cha kushukukia mikumi mjini aturudishie chenji yetu ule ujenzi ni zero, Iyovi pass not bad ile zile tutas loo, why tutas in the middle of nowhere?,Kitonga pass ni cancer level 4(mgonjwa anakufa sio kutibika),Chimala hadi Tunduma OSBP ni mbovu mno ,T2 kuanzia Nakonde hadi Isoka ni mix bag (inajengwa na ikiisha itakuwa super road),Isoka to Chinsali ni safi, na kati ya Chinsali to Serenje nayo ni mix bag,Ile bwawa la samaki limepigwa kifusi cha ovyo, na kutoka Serenje to kapiri ni safi,checks points za T1 hasa Sanga Sanga, Ruaha darajani ni pasta kichwa ,T2 zile za Chinsali, Mpika na Mkushi nazo ni Pasua kichwa, Dar to Moro ni lazima tufanye maarifa ya kupunguza traffic jam, like malori yapewe muda maalum wa kusafiri kwenye kipande hiki, thanks
Dar Moro wasipofanya kitu kuna siku foleni itakamata watu 48hrs. Kuna siku watu washakaa kuanzia saa4 usiku hadi 11 asubuhi na siku ingine tano usiku hadi 11 asubuhi.
Dawa ni expressway ya kulipia waliyoizungumzia ijengwe na zile njia sita kimara-kibaha zifike Morogoro.
Tatizo wenye maamuzi hawana exposure. Kama imewezekana kujenga sgr inashindikana kujenga proper highway?
 
Offroad nazikubali zaidi Landrover 110. Niliwahi kukuta mto umetema huko Manyara gari kibao zimepaki wanasubiri mto upungue.

Kufika pale kucheki maji hayana kasi, nikatia 4wD, Lock diff na Low range. Nikaingia nzima nzima chuma ikaogelea nikatoka upande wa pili.

Jamaa mmoja wa Landcruiser akaona kumbe simple tu nae akafata ila hakutoboa akakaa karibia na kutoka mwishoni.

Ilibidi nirudi tena humo humo kwa reverse nikasimama nikampiga belt na kumkokota hadi ng'ambo. [emoji1373][emoji1373]

Ukiachana na hilo tukio pia kuna sehemu nyingi sana nimewahi kuwakalisha wenye LC's tena kwenye tope ndio usiseme.

View attachment 2522538
Kuna kitu una mtafuta Extrovert ila nakushauri usiyajaribu maji.
 
Dar Moro wasipofanya kitu kuna siku foleni itakamata watu 48hrs. Kuna siku watu washakaa kuanzia saa4 usiku hadi 11 asubuhi na siku ingine tano usiku hadi 11 asubuhi.
Dawa ni expressway ya kulipia waliyoizungumzia ijengwe na zile njia sita kimara-kibaha zifike Morogoro.
Tatizo wenye maamuzi hawana exposure. Kama imewezekana kujenga sgr inashindikana kujenga proper highway?
Ile barabara kama unasafari yako ya kwenda mikoa ya mwanza au mbeya ukifika moro ndio ushukuru mungu kuna siku nimetoka dar nimeenda kulala vigwaza
 
Dom-Iringa-Dom [emoji108]
Screenshot_2023-02-19-18-56-44-342_com.google.android.apps.maps.jpg
 
Back
Top Bottom