Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Mwachie 10 ya pole.
Nimerudi tena kuweka mafuta pale pale,yafuatayo ndio mazunguzo yangu na Yule dada
Mimi:Mambo
Yeye😛oa
Mimi:Niwekee 15,000 (huku nampa20,000)
Yeye:Naomba uangalie kabla sijaanza kuweka nishakukariri
Nikatabasamu na yeye akacheka
Yeye:Siku ile mshale ulipanda
Mimi:Ulipanda ni kweli uliniwekea mafuta
Yeye:Ulijisikiaje
Mimi: Nilijisikia vibaya sana ndio maana leo nimekuja tena kwako nikuombe msamaha
Yeye:Mimi nimekusamehe (huku akinirudishia chenji 5,000)
Mimi:Asante hio chenji kaa nayo ni sehemu ya msamaha wangu.
Nilimuacha ametabasamu na roho yangu imetulia.
 
Uko vizuri sana MzeeBaba. Kwa kutoa Tips uko vizuri sana. Nimekubali.[emoji108]
 
...bado jambo moja hujafanya....fanya kubadilisha namba za simu...ndiyo mmeshakuwa friends hivyo..[emoji1][emoji1]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…