Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Unajua nimeanza kusoma hii comment yako kabla ya kuangalia hiyo clip
Sasa nilipoiangalia hilo basi lilivyokuwa linapepea imebidi nicheke tu
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Unajua nimeanza kusoma hii comment yako kabla ya kuangalia hiyo clip
Sasa nilipoiangalia hilo basi lilivyokuwa linapepea imebidi nicheke tu

Yaani na limepepea kwelikweli si mchezoo...

Wakati naanza kuiangalia hiyo video, jinsi basi lilivyoovateki, nilijua zile video game za kuendesha magari....

Nilipoona hii gari ndogo inavofukuza basi, nilijihisi niko ndani ya gari ndogo...

Niseme ukweli, nilijikuta nakanyaga breki hewa... 😁😁😁.
 
Mwisho wa mwaka 2023 sikuweza kusafiri nilikuwa busy na ujio wa Jr.
Hopeful 2024 tutapiga trip na Jr.
In fact road trip ya mwisho wa mwaka 2022 ndio Jr alitengenezwa
😎😎
 
Heri ya mwaka mpya RRONDO , nafurahi kukuona baada ya ukimya wa muda.

Nipe code niende Kwa speed Gani mafuta yasiende sana? Nimeshawakiwa na taa ya mafuta ikikaribia kuwa empty nikifika Dodoma kutokea Dar. Hapo ni Kwa speed ya 100-150.

Kwa Sasa nipo Mwanza nataka nirudi na njia ya kupitia Nzega-Tabora-Manyoni-Dodoma. Naona nikipiga full tank Mwanza ntatafuta Tena Kituo Dodoma.

Gari ni T5 XC 60. Ila Kuna wakati nilienda Moro na misele mingi Kwa speed ya 80-100 ilikua kutalii tu, full tank nilienda na kurudi na mafuta yalibaki.

Kwanza hiyo barabara ya kupitia Tabora si Iko shwari?
 
100-120kph ni nzuri sana. Lakini hio T5 kutembea mwendo wa kizee ni matumizi mabaya ya rasilimali.
Sahau mafuta have fun enjoy the ride
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…