Tena kifua chenye turbo mbili za maana. Ikiamsha hiyo chuma mpaka ardhi inatetemeka kama simba dume.
Na inanwaga moto vibaya mno, naomba pigia mstari neno vibaya mno na ujipige tano kifuani kuonesha heshima. Ukiizimua inachutama kama chura kudadadeki. Hii chuma kupiga overtake gari 10 zilizojipanga ni chap kwa haraka. (don't try this)
Hapo ukitoka nayo mpaka Dodoma hakuna gari inafuata kuanzia lc300 zote hata iwe ya petroli au hata crown majesta labda uwe na porsche and the like ndio utaweza kwenda nae sawa.
Hizi ndio zile gari wazungu wanasema," Tell me you're rich without telling me that you're rich". Kwa tafsiri isiyo rasmi kwamba,"Niambie wewe ni tajiri bila kuniambia kwamba wewe ni tajiri".
Iheshimiwe Brabus G800. Bima tu ya gari ni almost milioni 43-50, kwa hesabu za madafu mpaka kutua bongo ni kama milioni 900+ au bilioni 1 na ushee hivi.