Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Na ndo barabara yenye matuta mengi kuliko yoyote hapa nchi,idadi ya matuta inazidi idadi za kilometa za barabara
Yes, Tunduma hadi Sumbawanga ni kilomita 225 hivi, matuta yapo kama 220 hivi hapo bila kuhesabu rasta!

Ila nilivyopita siku chache zilizopita, niliona kama kuna baadhi ya matuta yameondolewa, ila bado yapo mengi sana.

Wazee wa kumaliza 'kisahani' panawafaa ila utamu unakatishwa na tuta la kufa mtu.
 
Kwa jinsi wanavyopenda sifa yakikauka watayapendesha tena ili tuzidi kukereka
Mkulu alishasema yakipungua ukubwa yasiongezwe tena.

Nilifanikiwa kupita njio hiyo wakati ikijengwa kabla lami haijafika Sumbawanga.

Kulikuwa hakuna matuta kama yaliyopo sasa bali kulikuwa na rasta tu, tena zile rasta za kuchimbwa chini, hivyo gari hupita vizuri tu na kutetema kidoogo kuashiria kivuko cha wenda kwa miguu mbele.

Lakini baada ya kukamilia yakawekwa matuta ya kufa mtu.

Eeee, walikuwa na sababu nzuri ya kufanya hivyo, ajali zilikuwa nyingi za magari kuanguka na pia ajali za wanavijiji kugongwa mara kwa mara.

Ni jambo la kawaida sana ukipita hata saa tisa za usiku kukuta wanakijiji wamekaa ama kusimama katikati ya lami wakipiga stori. Yani wamekufa wengi kwa kugongwa.

Ila kwa miaka hii tayari wanavijiji wamejifunza, hivyo hakuna haja ya kuwekwa matuta meeeeengi kama ilivyo bali yaachwe machache tu sehemu muhimu lakini alama na michoro ya barabarani iongezwe.
 
Duh nimevuta picha umejiachia ghafla unakuta kundi la watu katikati ya barabara!
 
Kujaza matuta barabarani ni ushamba mkubwa sana.
 
Hao wana vijiji wanafuata nini barabarani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…