Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Njia ya kuelekea Marangu
👍👍👍.
Marangu mtoni.

Kuna wachaga nilikuwa nafanya nao kazi, nilikuwa nawatania hatari kwa salamu za kichaga.....😅😅 kuna dada wa Kihaya pia wakati nasoma A Level alikuwa ananipenda alitaka niolewe na kaka yake. Basi akawa ananifundisha Kihaya....😜😜😜

Akili za Kasinde sasa.... nani anataka kunshutama na katweereerwoo....😁😁😁

Tangu hapo nikizoeana na mhaya namtania hadi anakuwa mpole...😅.

Basi tuu akili za Kasinde, uzuri wake walikuwa hawakasiriki.
 
Bibi ulitisha sanaa
 
Mkuu barabara zote za Tanzania usiku ni kama kucheza kamari Tu...jaribu kutoka DAR usiku kwenda DODOMA hapa unaweza kupaki pembeni ukasubiri asubuhi ufanye Safar
 
Nchi salana hii, trip piga muda wowote ukipata breakdown lala popote 🤣
 
Nchi salana hii, trip piga muda wowote ukipata breakdown lala popote 🤣

Uuweeeh....!!! Mi licha ya umri kusonga namuiga Baba Bataringaya 🙌.

Nimestaafu mambo ya kiza kinene, nyie endeleeni kutuwakilisha.

Wee lile giza la kwenye yale madaraja ya kati ya Bagamoyo na Msata unalionaga.....

Halafu ile siku napita sikupishana na gari yeyote toka Msata hadi nafika kituo cha mafuta BP, weeeh.... sina hamu.

Wakati najaza mafuta tena ile usiku mnene pale BP nilikuta Nissan Patrol zile tinted (za kazi maalum za kiserikali) niliitambua haraka japo ina plate namba za kawaida.

Dereva alikuwa ananitolea macho yenye maswali ila hana namna ya kuniuliza....

He was like, wewe mwanamke, usiku wote huu unatoka wapi, halafu nilivokuwa nimevaa sasa.... kilemba gauni kama dera ila linaishia magotini, viatu chachacha za ngozi soli ya mpira ile inakunjika kama silicon....🤪🤪🤪

Nikawa najinyoosha maana ndo sehemu niliona salama kushuka tangu kuanza safari Tanga, kisha huyooo nikamalizia safari hadi kitongojini nikapumzisha Bange za Kasinde.
 
yan ulikuwa mtu wa kaz kaz. Haha haaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…