Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Road trip kama Passenger
 

Attachments

  • 20240524_233028.jpg
    20240524_233028.jpg
    2.8 MB · Views: 14
Tuwe makini nyakati zote za usiku, kicheche kinaweza kukuletea majanga hata kama hakipo upande wako. Segera hiyo mida yetu ya kutawala
View attachment 3000155
Mkuu naona Hadi night Kali unamwaga Moto Tu...Ila usiku ni hatari sana kuendesha gari ingawa kuna Raha Sana,
Kwenye hiyo clip naona mwenye roli alikuwa anakuuzia mauti
 
Mkuu naona Hadi night Kali unamwaga Moto Tu...Ila usiku ni hatari sana kuendesha gari ingawa kuna Raha Sana,
Kwenye hiyo clip naona mwenye roli alikuwa anakuuzia mauti
Hamna moto humo itakuwa video tu. Spidi ya kawaida sana ndio maana nimeweza kurekebisha kosa lake kirahisi. La sivyo ningepeleka gari zima kichakani likachimbe dawa.

Jamaa alishatoa kichwa akaniachia body nihangaike nayo.
 
Usiku kuna mambo sana. Kuna zile barabara hazina mistari, so hujui mtu kajaa kwako au uko nje yaani hatari
Na awe anakupiga mataa full kama huyo wa lori hapo. Huoni lolote.

Nadhani kuna asilimia flani za imani zinahusika, mnapishana mnaamini tu hamtagusana na kweli hamgusani. Kuna barabara nyembamba ukitetemeka mkono kidogo mnavaana au unatoka nje.
 
Tuwe makini nyakati zote za usiku, kicheche kinaweza kukuletea majanga hata kama hakipo upande wako. Segera hiyo mida yetu ya kutawala
View attachment 3000155


Hao wenye Lori lililoharibika sio waungwana.....

Walitakiwa waweke matawi ya miti pande zote kuashiria gari zinazokuja kuna hatari wapunguze mwendo ili hata wanao overtake wawe kwenye mwendo mdogo hadi wapite eneo la hatari.

Kuna siku nilifanya safari ya hasira za mkizi, miaka kadhaa huko nyuma....

Kuna watu walinikera, mchana wa jua kali nikatoka kwenye kitongoji nilichopo kuelekea Bagamoyo. Saa nane mchana nikawa kituo cha mafuta BP pale baada ya round about.

Nikaweka full tank, nikaanza safari... niliingia Tanga mjini saa moja kasoro usiku. Nilipanga kulala, ila saa tatu usiku nikaanza safari ya kurudi Dar. Nilikunywa Redbull 2 macho yakawa kama fundi saa...
Nilikuwa nasimamishwa kwenye vizuizi vya checkpoint nashusha vioo, nasalimia wananiuliza unatoka wapi unaenda wapi najibu huyooo natambaa.... spidi inapunguzwa kwenye tuta tuu baada ya hapo ni kunyoosha goti.

Saa saba kasoro usiku niko tena kituo cha mafuta BP pale Bagamoyo kuweka mafuta maana mshale ulikuwa umelala empty.

Tanga sikuweka mafuta, niliingia kitongojini kwangu saa nane usiku. Sina hamu maana, kuna muda nilijuta kwanini niliendekeza hasira, ila kesho yake nikasikia raha kwa kuwa nilienda nikarudi salama.

Usiku mnene unatisha hasa ile barabara ya Msata Bagamoyo, kiza kinenee nikawa nawaza, nikipata pancha hapa ndo basi tena....😁.
Sikurudia na wala sitakaa nirudie tena huo mchezo.

Akili za Kasinde 🙂.
 
Kula Mabungo Baba Bataringaya, licha ya kuongeza nguvu za msuli wa kati, zinaimarisha macho na kuongeza uimara wa kuona mbali na karibu 🤪.
Dr kaniambia mambo ya umri tu.
 
Back
Top Bottom