Bongo hakuna Barabara za kuvimbia… Tunaendesha roho mkononi…
Machizi kibao barabarani, achilia mbali vichaa, wazee wa double kiki na vindoki vya msumbiji/malawi.
Mi yutong inayoendeshwa na vijana wasio acha mke wala watoto nyumbani…..”dereva asie na majukumu.”
Milori ilio skip service, yan mlori mpaka uue ndo uende service, madereva wanao sinzia hovyo barabarani… nadhani trip ya dar lusaka/ dar drc mnaifahamu vizuri…
Madereva wengine unakuta macho yashazoea kuaangalia nyuchi za malaya leo ndo utegemee kuziona road sign?
Dereva unakuta anamzigo wa majukumu ya kifamilia kuliko mzigo wa seruji alio ubeba…
Barabara yenyewe one way dar to kigoma, dar to manyara, dar to mtwara… mixer ubovu wa barabara.
Achilia mbali wale wazee wa naomba kadi ya gari, naomba lesi… ukiwa na elf 5 pembeni hata gari lisipo kuwa na steering wheel sio shida zao.
Inshort Tanzania hakuna road trip, ni death trip… so km huna ulazima wa kusafiri na private, hiyo pesa y fuel panda mwewe…✈️
Gari libaki tuu kwa misele y ndani y wilaya/mkoa. Mjane wako tutamuhifadhi, watoto je?
Tafakari chukua hatua. Haki Elimu