Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

😋😋😋😋😋
 
Kuna sehemu inaitwa Suji napo kuna wapare milimani wilaya ya Same ni balaa kuliko huko Usangi wenyewe wanapanda hadi Kwa miguu bila shida.
 
Sometimes God is super busy.

He can't pay attention all the time.

Don't be that reckless.
Tusipangiene basi ... 😀😀😀😀
Nipo baranarani na miaka kibao.. nimeisha kesha na gari miaka kiba.. hizi non stop ndio usiseme.. nimeisha jielewa vizuri zaidi.. na ndio maana na ushujaa wa kufanya ninachofanya.. na huku nikimtegemea Mungu
 
Kuna sehemu inaitwa Suji napo kuna wapare milimani wilaya ya Same ni balaa kuliko huko Usangi wenyewe wanapanda hadi Kwa miguu bila shida.
Wenyewe wanakwambia wanazoea hiyo milima.

Kuna jamaa amenionesha kiwanja amepewa na wazee wake.

Ni slope ambayo huwezi simama wima. Lazima utafute cha kujishikilizia.

Na anakwambia atajenga.

Ila upareni ujenzi ni gharama sana.

Usawazishe mlima mpaka upate kiwanja. Material unabeba kwa kichwa mpaka site. Ujenzi mpaka upasue miamba ndo msingi utokee. Maji unabeba kwa kichwa.

Ukijenga kwenye ile milima wewe mwanaume. Na nikaona na majumba ya hatari watu wamepaki alphard zao.

Wanasema tembea uone. Leo nimeona kwakweli.
 
Aisee....eti wanatafuta nini! Kule ndio wamepata maeneo huku chini kote kuna wenyewe
Hahaha inawezekana kweli mkuu

Lakini pia kuna watu wengine wanapenda tu kuishi milimani mtu anakwambia piga ua garagaza lazima aje kujenga milimani hata kama akuwe na maeneo mangapi huku chini tambarare ila lazima aje kuishi milimani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…