Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Hiki hutokeaga kwangu hasa nikichanganya sheli. Mara nyingi huwa naweka Total nikiwa mjini ila siku za safari huwa naweka wese la Lake oil full tank.
Sasa mara chache hutokea nataka niweke mafuta katika zone ambayo hamna total. Huwa sipendi kutembelea gari inayowaka taa ya mafuta hivyo nalazimika kuweka mafuta kwenye visheli uchwara kama Oilcom, Meru n.k Hapo ndio mziki sasa.
Gari yangu hunionyesha mabadiliko kwenye gauge after 1.5km distance maana nina katabia ka ku reset trip meter kila nikitoka sheli. Ikitokea haijafanya hivyo huwa nafadhaika sana na kuisi nimeibiwa hela bure kumbe wala inakuwa sio kweli.
 
Good RRONDO. Knowledge is power.
Kwa mujibu wa kanuni na sheria za usalama barabarani-matumiz ya Hazard kwenye Zebra siyo matumiz sahihi ya taa hizo.
Unakuta wakati mwingine mtu anawasha Hazard kwa sababu anataka kukatiza kwenye katikati ya barabara kwenda upande mwingine wa barabara,unamuuliza kwa nn unawasha Hazard anakwambia ili wengine wajue nataka kunyooka 😁 😁 😁 -Ukimuuliza umesoma wapi hzo kanuni hajui.Matumizi ya Hazard barabarani watu wengi hawayajui ikiwemo traffic wenyewe.
 
Hilo la tochi kituo A unasimamishwa kituo B bado linaendelea. Kuna siku maeneo karibia na Msata nilisimamishwa eti kwenye 50kph nimepita na 70kph. Nilikuwa na abiria na kila 50zone nilikuwa napita na 50. Wakanionesha picha. Ile picha inaonesha kibao kinachomaliza 50kph zone, nikamwambia nioneshe kibao cha 50kph zone ambako nimepita,hana picha. Nikamwambia mmetoa makusudi kibao cha kuanza 50kph ili watu wasikione halafu mnawapiga picha watu mkitumia kibao cha kumaliza 50kph mkiwatuhumu wako ndani ya 50kph zone na speed kubwa! Jamaa akawa mdogo akaniambia basi braza nenda.
Tulikuta gari nyingi pale zinapigwa faini,wengi hawakujua hii janja ya jamaa.
 
Mzee baba unaishi bongo kweli?

Hizo unazosema ni theories tu,mimi kipindi kile cha lugola amesema( sijui ukikutwa na kosa la taa ni mbovu,side mirror mbovu,rangi imeisha hilo ni kosa 1 tu la uchakavu na sio makosa matatu) nilikamatwa kule Tegeta nikiwa na kosa la taa 1 mbovu nikakuta traffic wamemshikilia jamaa mmoja ana harrier old model yuko anabishana nao huku amewatolea simu wale maafande kwamba Lugola anasema hivi na bla bla blah kibao.

Mimi walivyonifata nikawaambia ni kweli afande taa yangu kweli ni mbovu lkn kwa sasa siko njema mfukoni lkn w/end hii salary itaingizwa nitatengeneza afande,nikaomba samahani.

Afande akaniambia jitahidi uitengeneze na sikutoa hata senti,yule jamaa aliyekua anabishana nao mambo ya Lugola akaandikiwa makosa mawili na akaambiwa mpige huyo Lugola mwambie tumekuandikia na pia na No. ya RTO hii hapa mpigie huko mbele ya safari mueleze tumekuandikia kibabe maana tunapendaga wajuaji kama nyie.

Ninajua sehemu ya ku react na mipaka yangu inaishia wapi.
 
Naongelea sheria na miongozo ya nchi hii kaka na siyo hisia binafsi.
 
Hii walinibutua wale wa kagomeni mwembe chai pale... zebra haikuwa na mtu wala mnyama.. nikasema sawa andika.. roho iliniuma sana.. najua naonewa.. ila kwakua nilikuwa nimeisha kasirika sikuta hata kujieleza nikasema andika tu.
 
Hii walinibutua wale wa kagomeni mwembe chai pale... zebra haikuwa na mtu wala mnyama.. nikasema sawa andika.. roho iliniuma sana.. najua naonewa.. ila kwakua nilikuwa nimeisha kasirika sikuta hata kujieleza nikasema andika tu.
Sometimes unaepusha mengi kukubali kuonewa. Usiombe upewe kosa la kumzuia askari kufanya kazi yake!
 
Mtoto ulimkosha sana hapa lazima ulinyakua point 3 za ujentromeni😂
 
Changamoto hii kwa sehemu kubwa huchangiwa na shape ya tank la mafuta ya gari.Tank la gari naweza lifananisha na bakuli-nusu ya chini huwa inajaa haraha sana,lakini kadri unavyozidi kujaza upandaji wake kwanzia katikati kuja juu huhitaji kimiminika kingi zaid kujaa kuliko ile second half ya chini.Ndiyo maana kwenye baadhi ya magari Tank likizid half tunaonaga linachelewa kushuka kufika half,lakin likiwa chini ya half hushuka haraka sana.
 
Mtoto ulimkosha sana hapa lazima ulinyakua point 3 za ujentromeni😂
Alafu kwenye vituo vya mafuta ma manager wao huwa ni ma pisi kali.. tu.. hasa kama kituo flani.. nisikitaje .. muhusuki akawapo humu.. nikahamisha kambi bure 😀😀😀
 
Na hizo sheria na miongozo ndio jamaa wanapendaga watu wa dizaini hizo mzee.
RRONDO angeshalipa basi hiyo faini ya tochi aliyoambiwa kapigwa 😁 😁 😁 .Woga wako ni hasara yako-Pambania haki yako kwa hoja na siyo woga usio na msingi.Kama umeamua kuwa mkimya unapoonewa it's fine ni wewe,ila viongozi wa nchi wamesema hiyo hapana.Ukiona haki yako inakanyagwa waziwazi wametoa hotline upige and sometimes for freee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…