Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,379
- 41,294
Tip zao ile hela wanayopiga! Nitaanza kutoa tip
Yeah hata mia 5 kwao ni nauli tosha.
Ila mie sitatoa, si unajua hela ya mwanamke ilivyo chungu kutoka ππ
Ila huwa nawapigisha story ile ya kumtoa mawazo kama yuko kazini, asiwaze amesimama siku nzima labda kapata short au mwenzie anayetakiwa kumpokea shift kachelewa n.k.
Moja ya story naanzaga nazo ni, naweza kuwekewa mafuta ya buku huku nikionesha taswira ya wasiwasi na kushangaa...!
Wengi hucheka kisha nataja idadi ya lita nnazotaka basi maisha yanaenda.
Mmoja wakati anajaza nikamwambia, shoga hivi kama nimesahau pesa kwenye pochi nyumbani nilitoka haraka nanishaniwekea mafuta inakuwaje....
Basi akimaliza kunijibu hapo namwambia asante kwa huduma namtakia shift njema, akirudi nyumbani awakumbatie watu wake wa karibu kwa upendo. Namuacha na tabasamu halafu mie yuleee naendelea na safari yangu π.