Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Jamaa anawapa vichwa wenye passo, yani huku road kama una gari ya kiboya utadhaurika sana aseee[emoji23][emoji23]
Gari la kiboya ndo gari gani Mkuu?, nilikutanaga na ist road alinipita Hale tanga mi nikiwa na Subaru Forester jamaa alikaza Sana nilikuja kumpita mombo nikiwa 140 kph, Hawa jamaa wa ist , ukikutana na dereva mzuri anakuzalilisha hata Kama una gari la cc 3000 utazalilika tuu.
 
Sometimes it depends who is behind the wheel...
Hivyo usishangae hata Passo ya piston 3 ikiipita Crown..
 
Kama ulikuwa unaenda 100kph na yeye anaenda 120kph lazima akupite. Lakini Una cc3000 ukiamua hata dereva gani hakupiti na IST.
 
Hukuamua tu nawe!!!
 

Sijaelewa nahisi hapa, 140 ni speed kubwa sana? Mwendo wako wa kawaida huwa ni upi ambao ndio huwa unazalilishwa na hizo IST
 
Nilikuwa na tabia ya kufunga mkia kwenye high speed cars na Toyota Avensis Salon, toleo kwa ajili ya nchi za Ulaya, kisahani ni 260 Kph + 10

Muhimu ni kufunga tairi zenye kuhimili speed hiyo, (Masomo ya tyre speed code yapo mengi humu Jf)

Kawaida natembea 100kph, nikipitwa na gari kwa dharau, nami naunga tela, silipiti ila nahakikisha nipo nyuma yake hata afike 180kph.

Akizidisha 180kph ndipo huanza kumtafutia timing ya kumpita shaaa akiwa juu ya 200kph kisha mbele kidogo napunguza mwendo naacha apite halafu narudi na 100kph yangu.

Ligi zingine hata hazifai, hatari sana, nimekuwa mtu mzima sasa, da!
 

Ist hawezi nivimbia asee, univimbie nko na Ranger thubutuuu[emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…