Ijumaa
Nimetoka kabanga/ngara, nikiwa na tani 30 za maharage
Nimepanda k9 usiku wa saa 7 hadi benaco salama salimini, nikashuka mizani nyakatura, nikaenda kupumzika nyakanazi
Mapema tu nikalianzisha na P 360 kidot, kupitia mbogwe, runzewe hadi kahama, mzigo ukawa umecheza nikapanga upya
Toka kahama tinde, nzega, igunga singida nikalala manyoni Emirates pale..
Alfajiri nikalianzisha shusha salanda salanda bahi na dom kagua mzigo, gari shwari
Barabara ni safi kabisa hakuna utekaji wizi wala usumbufu
Shida ikaanzia kibamba hapo, vijana wakadandia wakachana turubai bahati nikaona, nikasimama nikaomba ulinzi shirikishi hapo hadi sokota, nikawalipa
Saa namalizia kushusha mzigo wa watu hapa temeke