Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Usiku mnene kipande kati ya Gairo na Dumila kuna ukungu wa kutisha. Ukiwasha full ndio huoni kabisa ukiwa na low beam unaona mita 20 tu mbele. Ukipishana na mtu inabidi uzime taa kwa muda utumie taa zake kuona.

Yani kwa kifupi kwenye ule ukungu inabidi upunguze taa kadiri uwezavyo. Ni balaa.

Huoni kingo za barabara. Inabidi utumie ile centerline kujiweka barabarani.
 
Gairo jana ilikuwa sana, kule njugwa ndio ilikuwa shidaaa yaani..ukungu unaenda kwa manyato
 
Hatare sana pole ndg!
 
Kipande cha Magubike na Tabu Hotel

Nadhani ile milima iliyo pembezoni
 
Ni sehemu mbili tofauti mkuu mwanga bar iko majengo mji mpya na chako ni chako ni kule airport!
Chombo ninacho operate hakiruhusiwi kupaki mjini, hapo hapo una king'amuzi

Hata ukipata breakdown tarura wanakufanya mradi

Kujua mitaa ya miji ni ngumu kidogo, ukiacha hiyo bambalaga iliyopo highway

Dodoma siifahamu,kivile
 
Asante wakuu. Nimetoka Dom saa 6 usiku, saa 11 kasorobo niko mjini. Dodoma sio mbali, basi tu.
Kweli mkuu sijui umetumia gari gani ila mfano kama LC V8 zina uwezo wa kutumia 4hrs tu from Dar to Dom ndiyo maana hata viongozi wakubwa wanaoendeshwa kwa hizi gari wana uwezo wa kuja Dar kila ijumaa jioni kuspend weekend nzima na kurudi Dom kila jumatatu asubuhi kuendelea na kazi! Wenyewe wanakuambia Dom hakujachangamka hivyo hapafai kula bata ndiyo maana wanatamani kurudi Dar!

Kuna siku Mwendazake alikuwa Mbeya na msafara wake imagine from Tukuyu to Mbeya mjini kwa gari za kawaida ni mwendo wa karibu lisaa na nusu lakini LC V8 za msafara wa Rais zilitumia nusu saa tu from Tukuyu to Mbeya! Yaani Mbeya mjini gari zote ambazo zilikuwa kwenye barabara ambayo msafara wa Rais ulitakiwa upite zilisimamishwa Mwendazake akiwa Tukuyu na baada ya nusu saa msafara ukawa umeshateremka Mbeya mjini!

Kwa sie SUV enthusiasts tunaona hapa kweli mjapan alitulia! Ndiyo maana binafsi kwa SUVs za mjep nazielewaga sana LC VXR V8 na NP Y62 V8 hizi gari huwa naziheshimu sana ni moto wa kuotea mbali!
 
Wanachotushinda hao ni kupita zone za 50kph na speed zaidi ya 100kph na kuovateki popote pale. Vinginevyo tungeenda nao Sawa tu.
Duh unazijua mashine sana
 
Wewe mkali [emoji3]

Unatembea na kupita mulemule kuzichambua na kuzielezea

Upo industry hii kitambo bhas
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…